2013 KCPE Kiswahili Past Paper-Free KCPE Past Papers with Answers.

THE KENYA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL

Kiswahili

Sehemu Ya Kwanza

Muda: Saa 1 dakika 40

Maagizo kwa watahiniwa

Soma maagizo yafuatayo kwa makini.

1. Umepewa kijitabu hiki cha maswali na karatasi ya kujibia. Kijitabu hiki kina maswali 50.

2. Ukiisha kuchagua jibu lake, lionyeshe katika KARATASI YA MAJIBU na wala sio katika kijitabu hiki cha maswali.

Jinsi ya kutumia karatasi ya majibu

3. Tumia penseli ya kawaida. 4. Hakikisha ya kwamba umeandika yafuatayo katika karatasi ya majibu:

Namba Yako Ya Mtihani

Jina Lako

Jina La Shule Yako

5. Kwa kuchora kistari katika visanduku vyenye namba zinazukuhusu, onyesha namba yako kamili ya mtihani (yaani namba ya shule, na zile namba talu za mlahiniwa) katika sehemu iliyolengwa mwanzani mwa karatasi ya majibu.

6. Usitic alama zozotc njc ya visanduku.

7. Iweke safi karatasi yako ya majibu na usiikunje.

8. Kwa kila swali 1 — 50 umepewa majibu manne. Majibu hayo yameonyeshwa kwa herufi A, B, C, D. Ni jibu MOJA tu kati ya hayo manna ambalo ni sahihi. Chaguajibu hilo.

9. Kwcnye karatasi ya majibu, jibu sahihi linnyeshwe kwa kuchora kistari katika kisanduku chenye herufi uliyochagua kuwa ndilnjibu.

Mfano

Katika kijitabu cha maswali:

21. Chaguajibu lenye ala za muziki pekee.

A. filimbi, udi, mvukuto, chapuo

B. njuga, tari, kinubi, fidla

C. harimuni, marimba, msondo. maleba

D. siwa. zeze, upatu. nembo.

Jibu sahihi ni B

Katika karatasi ya majibu:

1.[A] [B] [C] [D] 11.[A] [B] [C] [D] 21.[A] [B] [C] [D] 31.[A] [B] [C] [D] 41.[A] [B] [C] [D] Katika visanduku vinavyonnyesha majibu ya swali namba [2], kisanduku chenye herufi B ndicho kilichochorwa kistasi.

10. Chora kistari chako vizuri. Kistari chako kiwe cheusi na kisijitnkeze nje ya kisanduku.

11. Kwa kila swali, chora kistari katika kisanduku kimoja tu kati ya visanduku vinne ulivyopewa.

Kijitabu hiki cha maswali kina kurasa 7 zilizopigwa chapa.

Maswali 1 mpaka 15.

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15. Umepewa majibu marine hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Ufanisi wa mwanafunzi katika masomo humtegemea yeye. Licha ya kuwa mwalimu 1._ katika masuala mengi, uamuzi wa kuzingatia 2._ ya mwalimu huwa wake. Mwalimu hupitisha maarifa kama vile jinsi ya kutumia lugha kuwasiliana. Mathalani, mwalimu hufunza maneno kama vile halaiki, funda na kikosi ambayo ni 3._. Hali kadhalika, mwanafunzi hufunzwa maadili kama vile ustahimilivu ambao humfanya 4._. Ni dhahiri kwamba mwalimu ana uwezo mkubwa Wa 5._ mwanafunzi. Kwa hivyo hana budi kuwa kielelezo kifaacho kwani 6._. Mwanafunzi naye asiwe mlegevu, 7._.

1. A. humjuza

B. humwelekeza

C. humtambulisha

D. humtahadharisha

2. A. ilani

B. maafikiano

C. nasaha

D. matangazo

3. A. nomino za wingi

B. nomino za jamii

C. nomino za dhahania

D. nomino za jumla

4. A. kuwakubali Wenginejinsi Walivyo

B. kuwaamini wengine jinsi walivyo

C. kuwa rafiki mtiifu jinsi Walivyo

D. kuwa rafiki mpole jinsi walivyo

5. A. kumshawishi

B. kunishawishi

C. kujishawishi

D. kukushawishi

6. A. mtoto kwa mama hakui

B. mwana hufuata kisogo cha nina

C. sikio halipiti kichwa

D. chanda chcma huvikwa pete

7. A. awe na nia ya kujiimarisha masomoni

B. awe na hakika ya kujiimarisha masomoni

C. awe na ari ya kujiimarisha masomoni

D. awe na matumaini ya kujiimarisha masomoni

Ukosefu Wa mvua 8._ madhara yasiyomithilika. Ukame unapojiri wanyama na mimea 9._ Zaidi na joto. La muhilnu kujiuliza ni je, ikiwa Wa_nya.ma wanaathirika hivyo,10._ binadamu? Mojawapo ya 11._ hali hii ni hulka ya binadamu ya kutozingatia suala la kuongeza 12._ katika mazingira kwa 13._ Matokeo ya hulka hii ni kwamba watu wcngi wameshindwa 14._ hata kwa mahilaji ya kimsingi kama vile chakula. Wengine wanakuwa maskini ombaomba kwa kuuza ardhi yao 15._.

8. A. imesababishia

B. imesababisha

C. umesababisha

D. umesababishia

9. A. ndipo inayoathiriwa

B. ndivyo inayoathiriwa

C. ndio inayoathiriwa

D. ndiyo inayoathiriwa

10. A. lau

B. bali

C. ilhali

D. seuze

11. A. kiini cha

B. hatima ya

C. hatima za

D. viini vya

12. A. dhima

B. thamani

C. ustawi

D. hazina

13. A. kuitunza

B. kuyatunza

C. kuzitunza

D. kulitunza

14. A. kujitosheleza

B. kujiendeleza

C. kujilinda

D. kujilea

15. A. tepetepe

B. kijuujuu

C. lifutifu

D. kiholela

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

16.Chagua kielezi katika sentensi ifuatayo:

Mwanafunzi hodari na mtiifu aghalabu huwapendeza Watu wengi.

A. hodari

B. aghalabu

C. mtiifu

D. wengi.

17.Ni sentensi ipi ambayo imetumia ‘kwa‘ ya kuonyesha jinsi ya kufanya jambo?

A. Mchinjaji alikata nyaMAa kwa kisu.

B. Mwalimu alinipa alama nane kwa kumi.

C. Mwanafunzi amemwamkua mwalimu wake kwa heshima.

D. Mkimbizi alituzwa kwa kushinda mbio hizo.

18. Chagua usemi wa taarifa wa:

“Kwa nini mnamwajiri mtoto mdogo?” Afisa Wa Maslahi ya Watoto aliuliza.

A. Afisa wa Maslahi ya Watoto alimuuliza kwa nini alimwajiri mtoto mdogo.

B. Afisa Wa Maslahi ya Watoto alimuuliza kilichomfanya amwajiri mtoto mdogo.

C. Afisa Wa Maslahi ya Watoto aliwauliza kwa nini alimwajiri mtoto mdogo.

D. Afisa wa Maslahi ya Watoto aliwauliza kilichowafanya wamwajiri mtoto mdogo.

19. Chagua wingi wa: Hakujua kuwa mwashi angemjengeajumba kama hilo.

A. Hawakujua kuwa waashi wangewajengea majumba kama hayo.

B. Hamkujua kuwa waashi wangemjengea jumba kama hilo.

C. Hamkujua kuwa waashi wangewajengea jumba kama hilo.

D. Hawakujua kuwa waashi wangemjengea majumba kama hayo.

20. Tegua kitendawili

Kikigongwagongwa wanawe hutoka nje.

A. kichuguu

B. ngoma

C. nazi

D. hindi.

21. Chagua jibu ambalo lina vihusishi pekee.

A. halafu, tena, juu ya, kumbe;

B. ili, minghairi ya, wala, kama;

C. karibu na, tangu, katika, kuliko;

D. hatimaye, baina ya, bila, ama.

22. Maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo ni: Mzazi wangu amefika lakini wako atafika kesho.

A. kiclezi,kiwaki1ishi;

B. kivumishi,kiwaki1ishi;

C. kiwakilishi, kivumishi;

D. kivumishi, kielezi.

23.Chagua sentensi ambayo ina matumizi ya kiambishi ‘ki’ cha Wakati pekee.

A. Mwalimu akinipongeza nitafurahi sana.

B. Mwalimu alipofika shuleni alimkuta akisoma.

C. Chumba hiki kimepambwa vyema.

D. Mjomba Wangu hupenda kuvaa kizamani

24. Neno ‘mkwajuni’ lina silabi ngapi?

A. 3

B. 8

C. 4

D. 5

25. Watu Wenye majina sawa huitana:

A. umbu

B. babu

C. somo

D. shoga.

26. Koo ni kwa jimbi, _ ni kwa buda.

A. ajuza

B. binti

C. mseja

D. ghulamu

27. Sayari kubwa sana kuliko zote ni:

A. mshtarii

B. zebaki

C. zohali

D. utaridi.

28. _ ni kwa mekoni na shubaka ni kwa sebule.

A. takia

B. bembea

C. hodhi

D. kichanja.

29. Chagua methali ambayo inaafikiana na maelezo yafuatayo: ‘Tunapaswa kujishughulisha na mambo ambayo yanaonyesha dalili za mafanikio.’

A. Mtu hula nguvuze.

B. Mtu huenda na uchao, haendi na uchwao.

C. Mtu hujikuna ajipatapo.

D. Mtu hupata ajaliwalo, silo alitakalo.

30.Ukubwa Wa sentensi: ‘Kidole kirefu kimevikwa pete,’ ni:

A. Dole refu limevikwajipete.

B. Vidole virefu vimevikwa pete.

C. Dole refu limevikwa pete.

D. Vidole virefu vimevikwa jipete.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 — 40.

Maridhia alikuwa pale jukwaani akiwa miongoni mwa waalikwa mahususi katika shule ya upili ya Wasichana ya Twapambazuka. Hii ilikuwa shulc ya kipekee iliyokuwa imejengwa hivi majuzi kutokana na michango ya wafadhili na marafiki fulani Wa chanda na p<:t€ Wa Maridhia. Maridhia alipokuwa pale jukwaani aliwatupia macho wanafunzi waliokuwa wamejaa pomoni pale ukumbini. Kisha akajisemea kimoyomoyo, “Wanafunzi hawa wana bahati ya mtende. Wangejua kilichowapata wasichana wa enzi Zetu, katu Wasingezcmbca masomo. Wangcjua hatua kubwa iliyopigwa na dada Zao wangewaiga na kuzidi kufungua macho na kuikumbatia hamu ya kusoma Zaidi Sijui nitatumia lugha au mbinu gani leo kuwahamasishal” Rafikiye Maridhia, aliyekuwa mmoja wa wagcni, alipornwona Maridhia kadidimia mawazoni alimgutusha.

“Heel Maridhia, mbona hivyo? Unawazia nini?” Maridhia aliyaficha machozi yaliyokuwa yanayaziba macho yake, machozi yaliyotokana na kumbukumbu ya yale aliyoyapitia hadi kufikia pale. Kisha akajutia purukushani na kumjibu, “Hakunajambo la maana la kuwazia sasa. Ya kale hayanuki. Sasa nataka nigange yajayo.” Wakaendelea kusikiliza hotuba hizi na zile za kusifu hatua mbalimbali Zilizopigwa katika kuinua kiwango cha climu cha Wanawakc pale pao Shimoni. Mara kwa mara Maridhia alisikia jina lake likitajwa na kumiminiwa sifa kemkem na shukrani tele.

Maridhia alizirudisha fikira zake nyuma tena, akakumbuka vile alivyosoma kwa shida licha ya kuwa wazazi wake hawakuwa Wachochole. Alikumbuka vile wazazi hao Walivyoinnyima fursa ya kujiunga na shule ya upili kwa kufuata misimamo hasi ya wakazi wa Shimoni Wa Wakati huo. I-lawa Waliandama fikira kuwa kumsomesha msichana ni kupoteza mali bure. Wazazi wa Maridhia, kwa kuongozwa na tamaa, wakamuoza kwa babu mmoja mkwasi kupindukia. Ilibidi Maridhia akubali uamuzi huu shingo upande. Maridhia alikumbuka jinsi alivyotescka katika ndoa hiyo. Alikumbuka vipigo vya kila mara, vicheko, vitisho na kuaibishwa hadharani na jamii, hasa ilipotokca kuwa amechelewa kuipata mbeleko.

Mambo yalipomfika kooni akasema, “Polelea mbali, liwe liwalo, hata wakisema mwacha mila ni mtumwa ni sawa. Maneno matupu hayavunji mifupa.” Baada ya kuwaza na kuwazua Maridhia alitafuta maarifa ya kujinasua, akamwendea Bi Salama na kumlilia shida. Bi Salama alimshauri ajiunge na kituo cha elimu ya Watu Wazima. Huko Maridhia alipewa mafunzo mengi. Alitia shime masomoni akiamini kuwa kisomo hakina umri Wala mwisho, akasoma hadi chuo kikuu. Baada ya kuhitimu chuoni alirudi kwao na kupata kazi ambayo ilimwczesha kuwakimu wazazi Wake waliokuwa wazee.

Aidha alianzisha miradi mbalimbali Shimoni. Mafanikio ya Maridhia yaliwasula na kuwaaibisha kindanindani wale waliomdhulumu awali. Wengine walimsingizia hili na lile. Hata hivyo, hawangewcza kufanya lolotc kuizima kiu ya Maridhia ya kujiendeleza. Maridhia aliwapuuza akisema kuwa asilani jua haliwezi kuzuiwa kwa ungo. Miaka mitatu baada ya Maridhia kupata kazi Walimdiana na mumewe. Mumewe alimwomba msamaha naye Maridhia akamsamehe. Aliwasamehe pia wote waliomtesa. Aliwaona kuwa Walioongozwa na itikadi Zilizopitwa na wakati.

Aliwaelirnisha wanakijiji kuwa ni muhimu kumsomesha mwanamke pia. Wasibague. Mwanamke mmoja akielimishwa, huelimisha dunia. Maneno ya Maridhia yalimtoa nyoka pangoni, watu Wakawasomesha Wana Wa jinsia zote, Shimoni ikaanza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Shule zilijengwa, miundomsingi kama vile barabara ikaimarishwa na hospitali zilizokuwepo zikaboreshwa. Maji ya mabomba yalisambazwa vijijini, chombo kilichokuwa kinaelekea kuzama kikaokolewa.

Sifa za Maridhia zilivuma pembe zote za Shimoni na jamii jirani. Wazazi na Walezi waliwapigia watoto wao mfano wa Maridhia ambaye aliweza kuzikosoa mila duni na akafaulu. J ambo hilo lilionekana kuwa inwiko hapo awali. Jamii nzima ilifunguka macho; Maridhia akawa kiclelezo, si kwa vijana wa kike tu, bali pia kwa vijana Wa kiume, wazazi najamii kwajumla.

31. Wanafunzi Wa Twapambazuka

walibahatika kwa vile:

A. shule yao ilikuwa ya kipekee;

B. shule yao ilikuwa imefadhiliwa;

C. hawakubaguliwa kimasomo kama awali;

D. hawakupatwa na kilichowapata wenzao.

32. Machozi ya Maridhia yalitokana hasa na:

A. kumbukumbu ya mateso aliyokuwa anapitia;

B. kumbukumbu ya talaka na ndoa yenye taabu;

C. kumbukumbu ya mateso Waliyopitia na wenzake;

D. kumbukumbu ya mateso na mafanikio yake.

33. Wazazi wa Maridhia walikiuka haki gani za watoto?

A. upendo, maarifa;

B. utulivu, heshima;

C. hiari, elimu;

D. shime, usalama.

34. Chagua msimamo Wa rnwandishi kuhusu elimu.

A. Huweza kupatikana kipindi chochote na katika daraja lolote.

B. Huweza kupatikana na mtu yeyote na mahali kotekote.

C. Huweza kupatikana baada ya kujiunga na kituo cha elimu.

D. Huweza kupatikana na Watu Wazima baada ya kujinasua.

35. Ni sifa zipi zinazoafiki zaidi jamii ya Maridhia?

A. ubinafsi, uongo, ushirikiano, maridhiano;

B. ukatili, ubaguzi, umoja, maridhiano;

C. tamaa, woga, dhuluma, maridhiano;

D. ulaghai, usalama, husuda, maridhiano.

36. Kijiji cha Shimoni kilikuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya:

A. kufuata sana tamaduni na mila zao;

B. kupuuza mchango Wa vijana katika maendeleo

C. kutowazia Wito wa vijana kuhusu maendeleo

D. kuwatia wasichana katika ndoa Za mateso.

37. Mafanikio ya Maridhia yaliwezesha raia Wa Shimoni;

A. kujenga hospitali nzuri Zaidi na kukuza elimu;

B. kupanua barabara na usawa;

C. kusambaza maji na elimu;

D. kustawisha vijiji na kuimarisha huduma za afya.

38. ‘Sifa za Maridhia zilivuma pembe zote za Shimoni na jamii jirani.’ Methali inayoweza kujumuisha maneno haya ni:

A. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.

B. Mkulima ni mmoja Walaji ni wengi.

C. Mkuu hukua kwao.

D. Mcheza kwao hutuzwa.

39. Maana ya: ‘kuipata mbeleko’, ni:

A. kujipatia mahitaji ya mtoto

B. kuwa na matumaini ya ujauzito; C. kujifungua mtoto;

D. kuwa mjamzito.

40. Chagua kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki.

A. Umuhimu wa miundomsingi;

B. Umuhimu Wa kusameheana;

C. Umuhimu Wa elimu;

D. Umuhimu wa ufadhili.

Soma kifungu kifimlacho kishu ujibu maswali 41 mpaka 50.

Amani ni hali inayofaa kuenziwa na kuimarishwa kila Wakati na kila mahali. Baadhi ya Watu huamini kuwa amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga lakini si kweli wakati wote. Amani ya kudumu huweza pia kupatikana kwa njia ya maafikiano. Ukosefu wa amani una gharama kubwa isiyolipika kwa urahisi. Wahenga waliosema, “Kama hujui kufa tazama kaburi,” hawakukosea. Tukitaka kuyajua maafa yaletwayo na vita katika ukanda huu, tuna mifano kcmkem. Si nchini, si kwa majirani, twaweza kujifunza mengi kuhusu umuhimu wa amani na hasara zinazoletwa na kinyume chake.

Jamii zinazokumbwa na mizozo hujionea makubwa. Baadhi ya Watu Waliowahi kuwa mamlakani huweza kupoteza nyadhifa zao; viongozi wa awali wakawa si chochote si lolote. Hali ya utulivu, furaha na maendeleo huloweka kama moshi. Mambo mengi hutumbukia nyongo. Uharibifu Wa mali hushamiri na Wengi hupoteza milki zao. Vurugu zinapotokea watu hutoroka, kila mmoja akikimbiza roho yake. Wakati kama huu, mali kama vile mashamba, majumba ya kifahari, magari mengi, pesa na hata mifugo huwa mizigo mizito isiyobebeka. Katika hali hii familia hujikuta zimesambaratika. Upweke nao huzidi. Pa kukimbiliwa pia huwa shida. Hali ya utegemezi huibuka. Wakimbizi hutegemea usalama kutokana na ukarimu na ukaribu uliopo kati yao na Wahisani Wao. Mambo hayawi sawa hata kidogo. Ghafia uhuru anaokuwa nao mtu hutoweka kwani cha mwenzio hakiwezi kuwa kama chako na huwezi kukitolea sauti, ni nguo ya kuazima ati.

Watu wakiwa uhamishoni ndipo wanapokumbuka umuhimu wa amani. Wao huj uta na kukumbuka mambo yasiyo na msingi yaliyozua ghasia. Wengi hukumbuka vurumai zilizotokana na tofauti kubwa za kisiasa, kiuchumi na kikabila, ufisadi na tamaa. Wengine huwaza kwa uchungu kuhusu hali ya mali za Walizochuma kwa miaka mingi kuangamizwa kwa sekunde chache tu! Wengi Wao hutatizika kimawazo Wasijue pa kuanzia Wala pa kuelekezea juhudi zao. lkumbukwe kuwa ukimbizi nchini au nje ya nchi ni karaha tupu. Mahitaji ya kimsingi kama vile chakula, maji, makao, mavazi na malazi hukosekana. Magonjwa hatari hukurupuka kila mara. lsitoshe vifo huzidi, sio tu kupitia magonjwa, bali pia kutokana na mapigano na dhiki za kisaikolojia .

Wakati huu, uvunjaji wa sheria huzidi na uchumi wa nchi huzorota kwani hata watalii huchelea kuingia nchini kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Fahari ya nchi hudidimizwa na kuzikwa kwenye lindi la kina kirefu. Ili kuhakikisha kuwa jamii zote zinaishi kwa amani, haifai kupakata mikono na kuamini kuwa Wazazi, Walimu na viongozi ndio ambao hawana budi kujaribu kwa hali na mali kuhubiria umuhimu Wa amani na kusameheana. lnatujuzu kujaribu kuibua na kukuza hisia za uzalendo miongoni mwa wanajamii. Elimu nayo ifunze na kusisitiza umuhimu wa kuwa raia wema. Raia wote waelimishwe kuhusu umuhimu wa kuzmdama sera na mienendo inayohimiza usawa katika makundi yole ya kijamii.

Walio katika mamlaka Wawasisitizie vijana umuhimu Wa kuungana na raia wcnginc licha ya tofauti zao za kikabila, kihali na hata kirangi.

41. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu.

A. Amani huweza kupatikana hata palipo na ugomvi.

B. Amani huimarishwa zaidi baada ya maafikiano.

C. Kuwepo kwa amani huwawezesha Watu kujifunza mengi.

D. Kwenye amani gharama ya vita hupungua.

42. ‘Kama hujui kufa tazama kaburi,’ ina maana:

A. Kama hulielewi jambo, chunguza matokeo yake.

B. Ikiwa hujawahi kukielewa kifo chunguza kiini chake.

C. Kama hukielewi kifo chunguza matokeo yake.

D. lkiwa huj awahi kuyaelewa matatizo chunguza chanzo chake.

43. Mashamba, majumba ya kifahari, magari mengi, pesa na hata mifugo huwa mizigo mizito isiyobebeka, kwa sababu:

A. Wakimbizi huwa na haraka;

B. wakimbizi huwa na wasiwasi;

C. Wakimbizi wanataka lnabadiliko;

D. Wakimbizi wanataka kujiokoa.

44. Kupokelewa kwa wakimbizi hutegemea hasa:

A. urafiki wa Wenyeji;

B. utu wa wenyeji;

C. udugu Wa Wenyeji;

D. ujirani wa wenyeji.

45. Kulingana na aya ya tano chanzo cha vurugu ni:

A. tofauti Za kisiasa na uchochezi;

B. tofauti za kisiasa na rangi;

C. kuwepo kwa ubinafsi na ubaguzi;

D. kuwepo kwa umaskini na ulajiri.

46. Uhamishoni

A. Watu hupoteza hadhi zao.

B. Watu hukurupuka kwa magonjwa.

C. Shughuli za kuzalisha chakula huzorota.

D. Shughuli za kudumisha watalii hupungua.

47. ‘Cha mwenzio hakiwezi kuwa kama chako na huwezi kukitolea sauti’. Chagua methali inayojumuisha maelezo haya.

A. Jogoo wa shamba hawiki mjini.

B. Bura yangu siibadili na rehani.

C. Kamba ya mbali huvutwa kwa uangalifu.

D. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.

48. Chagua athari za ukimbizi kwa mujibu wa aya ya sita.

A. Nchi hupoteza Walinda usalama.

B. Nchi hukumbwa na tatizo la kimawazo.

C. Nchi hupoteza pesa za kigeni. D. Nchi hukumbwa na tatizo la wawekezaji.

49. Kulingana na kifungu, jukumu la kudumisha amani:

A. linahitaji ushirikiano Wa Walimu na viongozi;

B. linahitaji ushirikiano wa raia wote; C. linahitaji ushirikiano Wa Wahisani na wakimbizi;

D. linahitaji ushirikiano Wa Wenye mamlaka kote.

50. Maana ya: ‘hushamiri,’ ni: A. huzoroteka;

B. hushangaza;

C. huumiza;

D. huongezeka.

2013 KCPE Kiswahili Past Paper-Marking Scheme/Answers

1 B

2 C

3 B

4 A

5 A

6 B

7 C

8 C

9 D

10 D

11 D

12 B

13 B

14 A

15 D

16 B

17 C

18 D

19 A

20 A

21 C

22 B

23 B

24 C

25 C

26 A

27 A

28 D

29 B

30 A

31 C

32 D

33 C

34 A

35 B

36 B

37 D

38 D

39 C

40 C

41 A

42 A

43 D

44 B

45 C

46 A

47 B

48 C

49 B

50 D