2021 Mock Kiswahili Paper 2 na Majibu-Kenya High School

UFAHAMU: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia

Mateso ya wanawakiwa ni suala la kijamii linalofaa kutazamwa kwa darubini kali.

Hata hivyo wanaoathirika zaidi ni watoto ambao bado wako katika umri unaohitaji kulelewa na kupewa mahitaji ya msingi kama mavazi, malazi, elimu na mengine anuwai.

Hali ya kuachwa na wazazi imekuwa ikizikumba jamii tangu enzi za mababu na kila itokeapo, wanajamii huipokea kwa mitazamo tofautitofauti, hivyo kuwafanya wanawakiwa kuathirika sana.

Baadhi ya jamii zina imani za kijadi pamwe na mila zilizochakaa zinazozifanya kuamini kuwa baadhi ya vifo hutokana na laana.

Wengine huchukulia kuwa mwendazake ameondolewa na ulozi.

Imani kama hizi huifanya jamii kuwatia watoto walioachwa katika mkumbo ule ule, hivyo kuwaangalia kwa macho yasiyo ya kawaida.

Hili husababisha dhana gande. Hali hii husababisha kuwachukulia watoto kama wanaotoka katika kizazi kilicholaaniwa. Jamii basi hukosa kuwapa watoto hawa stahiki yao. Hata wanapojitahidi kuiwania nafasi yao, waliowazunguka huwavunja mioyo. Jitihada zao huishia kuwa si chochote kwa kuwa jamii inawatazama kama waliolaaniwa.

Punde baada ya mzazi mmoja au wote wawili waendapo wasikorudi, inatarajiwa kwamba aliyeachiwa mtoto, awe mzazi wake, mwanafamilia au jirani awajibike na kumtunza mwanamkiwa. Kunao kadha wa kadha wanaowajibika – ninawavulia kofia. Hata hivyo wengi hutelekeza jukumu hili walilopewa na Muumba.

Si ajabu basi kuona kuwa idadi ya watoto wanaozurura mitaani inazidi kuongezeka kila uchao. Ukichunguza utakuta kuwa wengi wa watoto hawa ni waliopotelewa na wazazi wao.

Inakera zaidi kugundua kuwa baadhi ya watoto hawa wana mzazi mmoja.

Kwamba mke au mume wa mtu ameaga, au iwe kwamba mzazi mmoja alimzaa mtoto na kumwachia mwenzake mzigo wa ulezi, aliyeachiwa ana jukumu la kumpa mwanawe mahitaji ya msingi. Machoni pa Jalali, kila anayeupuuza wajibu huu ana hukumu yake siku ya kiama! Ni haki ya kila mtoto kupata elimu. Katika katiba ya Kenya mathalan, elimu ya msingi, yaani kuanzia shule ya chekechea had kidato cha nne ni ya lazima.

Tangu hapo hata hivyo, jamii zimekuwa zikiwanyima wanawakiwa wengi elimu. Kwamba kunao wachache wanaowaelimisha baadhi ya wanawakiwa, ni kweli.

Hata hivyo, wengi hukosa hata wa kuwapeleka katika shule ya chekechea, hivyo kuishia kutojua hata kuandika majina yao.

Mfikirie mtu katika karne ya 21, asiyejua kusoma wala kuandika! Nani ajuaye, huenda huyo mwanamkiwa asiyepelekwa shuleni ndiye angalikuwa profesa, daktari, mwalimu, rubani au msomi mtajika na mtaalamu wa uwanja muhimu katika jamii!

Kila mtoto ana haki ya kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito. Katika katiba ya Kenya, utu uzima, ulio umri wa kuanza kufanya kazi huanzia miaka 18.

Wanaohakikisha watoto hawa wametimiza utu uzima kabla ya kufanyishwa gange ngumu wanafaa pongezi.

Hata hivyo wanawakiwa wamekuwa wakitumiwa na wengi kama punda wa huduma.

Wanaaila wengine huwachukua wanawakiwa kwa machozi mengi wazazi wao waagapo nakuapa kuwahifadhi na kuwatunza wana wale wa ndugu zao, kumbe ni machozi ya simba kumlilia swara! Hata kabla ya mwili wa mzazi mhusika kuliwa na viwavi, mateso kwa mtoto yule huanza, akawa ndiye afanyaye kazi zote ngumu.

Utakuta watoto wao wamekaa kama sultan bin jerehe huku mwanamkiwa yule akiwapikia, kuwafulia nguo, kudeki, karibu hata awaoshe miili! Kazi kama zile za shokoa huwa za sulubu na aghalabu husindikizwa kwa matusi yasiyoandikika.

Baadhi ya waja walionyimwa huruma huwahadaa wanawakiwa na kuwapeleka ng’ambo wakitumia vyambo, kuwa wakifika kule watapata kazi za kifahari.

Maskini wale hushia kushikwa shokoa, wakawa watumwa katika nyumba za waajiri wao, bila namna ya kujinasua. Wengine hushia kutumiwa kama watumwa wa ‘kimapenzi’ katika madanguro, miili yao ikawa ya kuuziwa makahaba waroho wasiojali utu.

Kujinasua kule huwa sawa na kujitahidi kuokoa ukuni uliokwishageuka jivu, maadamu wanawakiwa aghalabu hukosa watu wenye mioyo ya huruma ya kuwashughulikia.

Wengi huitumia methali ‘mwana wa ndugu kirugu mjukuu mwanangwa’ kuwapuuzilia mbali wanawakiwa ambao hukimbiliwa tu wabinafsi hawa wanapofaidika wenyewe.

Maswali

a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka. (alama 1)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

b) Eleza dhana ya mwanamkiwa kwa mujibu wa kifungu. (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

c) Eleza imani za kijadi kuhusiana na wanawakiwa. (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

d) Jadili masaibu yanayowakumba wanawakiwa. (alama 4)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

e) Eleza haki mbili za kikatiba zilizokiukwa kuhusiana na wanawakiwa. (alama 4)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

Eleza maana ya msamiati ufuatao kulingana na kifungu. (alama 2)

Inakera

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

Majukumu

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

UFUPISHO: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasiliano kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundishia.

Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkemu kwa mtu wa kila rika. Halikadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani.

Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji wa stadi ya kujifundisha au kujielimisha.

Michezo ya video, hasa ya kielimu, huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi. Fauka ya hayo, televisheni ni chemchemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha.

Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa.

Televisheni ni mojawapo ya vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro tunayokabiliana nayo kila siku. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu.

Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga huwa ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.

Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari.

Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya wa kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia, kabila na utamaduni.

Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanaowaacha takribani uchi wa mnyama.

Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga. Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga.

Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii.

Ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa ya kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.

Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalani, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, n.k.

Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.

Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya dawa za kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi.

Si ajabu mtu anapouliza wanaotumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.

Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote.

Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.

Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya wawaelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.

a) Fupisha aya tatu za kwanza za (maneno 70 – 75) (alama 7, 2 za utiririko)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

Jibu

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

Matayarisho

3.MATUMIZI YA LUGHA: (alama 40)

a) Taja aina mbili kuu za ala za kutamkia sauti (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

b) Taja mfano mmoja mmoja wa sauti zifuatazo (alama 2)

Kimadende__________________________________________________________

Kipasuo kwamizo_____________________________________________________

c) Huku ukitoa mfano, eleza maana ya sentensi sahili (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

d) Ainisha mofimu katika neno lifuatalo (alama 3)

Tulimpikia___________________________________________________________

e) Ainisha vitenzi katika sentensi: Kitabu anachotaka kusoma ki mezani (alama 3)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

f) Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi kiteuzi (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

g) Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani? (alama 2)

a) Uzi____________________________

b) Muda__________________________

h) Tumia ‘o’ rejeshi ya kati katika sentensi ifuatayo (alama 2)

Watu ambao walifika jana ni wale ambao walitoka mbali

____________________________________________________________________

i) Onyesha shamirisho kipozi na ala katika sentensi ifuatayo (alama 2)

Mwindaji haramu alimuua ndovu kwa bunduki

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

j) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia mistari au mishale (alama 3)

Kilipikwa jana jioni

_____________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

k) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi (alama 2)

Msingesoma kwa bidii, msingepita

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

l) Tunga sentensi moja kudhihirisha dhamira/jukumu hili (alama 2)< p> Rai/ombi

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ m) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (alama 2)

Mtoto ambaye alianguka jana ana maumivu mengi

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

n) Onyesha matumizi yoyote mawili ya kiwakifishi: koma/kituo (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

o) Tumia neno ‘Nairobi’ kama (alama 2)

a) Nomino

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

b) Kielezi

________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ p) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya kuku na gugu (alama 2)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

q) Onyesha matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi (alama 2)

Mwongeleaji stadi anajishaua sana.

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ ______________________________________________________________________________________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

r) Andika katika usemi wa taarifa (alama 2)

“Wageni wangu watafika saa ngapi? Mama aliuliza

______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ s) Unda nomino kutokana na kitenzi (alama 1)

Safari

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

ISIMUJAMII: (alama 10)

Nipe chai, andazi mbili na egg moja………….

a) Taja sajili inayorejelewa na maneno haya

(alama 2) _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

b) Fafanua sifa nne zinazohusishwa na sajili hiyo (alama 8)

_______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________ _______________________________________________________________________

Mwongozo Wa Kusahihisha Insha Karatasi 102/2

1.a) Wanawakiwa/mateso ya wanawakiwa. (alama 1)

b) Ni mtoto aliyefiwa na mzazi mmoja au wote. (alama 1)

c) i) Baadhi ya vifo hutokana na laana.

ii) Mwendazake ameondolewa na ulozi. 2×1=2

d) i) Wanatelekezwa na walioachiwa jukumu la kuwatunza hivyo kuishia kuwa watoto wanaozurura mitaani.

ii) Hawapelekwi shuleni

iii) Fanyishwa kazi ngumu

vi) Wanadaiwa na kupelekwa ng’ambo kuwa watapata kazi za kifahari lakini wanaishia kuwa watumwa wa kimapenzi 4×1=4

e) i) Haki ya elimu ya msingi

ii) Kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito

f) i) Inaudhi/inakasirisha

ii) Kazi/wadhifa

Adhabu

Sarufi – ½ x 6 s=3

Hijai – ½ x 6 h=3

2.a. i) Runinga ina manufaa yake

ii) Ni nyenzo mwafaka ya kufundishia

iii) Vipindi vinayopeperushwa huwa na mafunzo kwa kila mtu

iv) Huleta vipindi ambayo huwafahamisha watu mambo ambayo yanaendelea katika mazingira yao

v) Ikitumika pamoja na michezo ya video husaidia katika ukuzaji na ustawishaji wa stadi ya kujifundisha/kujielimisha

v) Michoro ya video huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuwafanya watu kuwa makini wanapofanya kazi

vi) Ni chemchemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha

vii) Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro

viii) Hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu

ix) Hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jami zozote 7×1=7

b. i) Baadhi ya vipindi hujumuisha ujumbe usio na maadili

ii) Vijana mengi wamekopa na kuyaiga wanayoyaona katika runinga

iii) Matumizi yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia

iv) Aghalabu hueneza maadili yasiyofaa

v) Baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya dawa za kulevya

vi) Ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi

Adhabu

Sarufi – ½ x 6 s =3

Hujai- ½ x 6 h=3

Ziada – maneno 10 ondoa alama 1 na kila maneno 5 ya ziada ondoa ½

3. a) Tuli

Sogezi

b)[r]

[ch]

2 x1=2 c) Ni sentensi iliyo na nomino (kiima) na kitenzi au kitenzi kikuu kimoja/sentensi inayobeba wazo moja tu. k.m. Mama anapika chakula

Maelezo 1

Mfano 1

d) Tu – li – m – pik – i – a Nafasi Kiishio – Wakati – Mtedwa – Mzizi – Kauli ½ x6=3

e) anachotaka –Ts (kitenzi kisaidizi)

kusoma – T (kitenzi kikuu)

ki – t (kishirikishi kipungufu) 3×1=3

f) Kadiria jibu

Ni viunganishi kama: au, ama, wala n.k (alama 2)

g) i) U –ZI ii) U – U

h) Watu waliofika jana ni wale waliotoka mbali (alama 2)

i) Ndovu – shamirisho kipozi

ii) Bunduki – shamirisho ala

2×1=2 i) S – KN+ KT

KN O

KT + E + E

T – Kilipikwa

E – jana

E – jioni

j) Mngesoma kwa bidii, mngepita sana 2×1=2

k) Kadiria jibu

Maneno kama: naomba, tafadhali n.k. yatumike (alama 2)

Mtoto ambaye alianguka jana/ana maumivu mengi tegemezi / huru

i) Hutumika pale msomaji anapohitaji kutua au kupumua

ii) Kutenganisha maneno katika orodha< p> iii) Katika tarakwimu zaidi ya elfu moja

iv) Katika kuandika anwani za kwanza 2×1=2

n) Kadiria jibu k.m.

i)Nairobi ni mji mkuu wa Kenya.

ii) Wanafunzi walienda ziara Nairobi 2×1=2

o) Kuku – ndege wa jamii ya kanga lakini mkubwa na anayefugwa

Gugu – majani yasiyohitajika katika shamba

( Kadiria sentensi)

2×1=2 p).i) Onyesha mtu anayefanya kitendo

ii) Rejelea nafsi 2×1=2

q) Mama alitaka kujua wageni wake wangefika saa ngapi? 2×1=2

r) Safari/kusafiri/msafiri/msafara 1×1=1

SARUFI

Adhibu kila kosa la kisarufi litokeapo kwa mara ya kwanza hadi nusu ya alama mtahiniwa alizopata katika kila kisehemu Kila kosa ni nusu alama

HIJAI

Ondoa nusu alama kwa kila kosa la hijai litokeapo kwa mara ya kwanza hadi makosa 3 ½ x6=3

4. a) Hotelini/mkahawani

b) i) Lugha si sanifu

ii) Kuchanganya ndimi iv) Sentensi fupi

v) Lugha ya heshima

vi) Lugha ya biashara

vii)Lugha ya ucheshi

viii)Matumizi ya jazanda

ix)Msamiati maalum k.m. meu n.k.