2015 KCPE Kiswahili Past Paper-Free KCPE Past Papers with Answers.

KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2015

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.

Chaguajibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Tanga hakujua maana ya jirani…….1…… siku……..2……… na ya kufika. Alikuwa ……3……. watu ambao…..4……….. kuwa Wakipatwa na tatizo, ndugu atawasaidia. Tanga alisahau kuwa ……5…….. …….6…… tatizo litakuwa ….7……… sana kabla huyo ndugu…………….8…………kufika.

1. A. kisha B. tangu C. hadi D. tena

2. A. aliyefikwa B. alipofikwa C. aliofikwa D. alikofikwa

3. A. katika B.kwenye C. kati ya D. baadhi ya

4. A. Wataamini B. Wangeamini C. wanaamini D. Wakaamini

5. A. fimbo ya mbali haiui nyoka wakaamini

B. mtegemea cha nduguye hufa maskini

D. heri nusu ya shari kuliko shari kamili

C. akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki

6. A. — B.; C.: D. !

7. A. limekuathiri B. limemwathiri C. limetuathiri D. limewaathiri

8. A. yako B. yetu C. yake D. yenu

Sikukuu za kitaifa ni muhimu kwa nchi….9…………………… Sikukuu hizi haziwaleti watu pamoja tu, ………………..10………pia huwa kumbukumbu ya matukio ya awali. Wakati huu si ajabu, yaani si ………………11… kuwaona………….. 12……………. wakipiga ngoma kwa ustadi mkuu huku vij ana wakikariri mashairi ya mishororo mitano katika

kila ubeti. Mashairi ya aina hii huitwa……………….. . Wakati huu kiongozi hutoa hotuba kwa taifa ili ……….14…………. kuandama mienendo …………………… .

9. A. lolote B.yoyote C. yeyote D. wowote 10. A. hata B.bali C. kwani D.wala

ll. A. shaka B. neno C. hoja D. ibra

12. A. manju B. ngoi C. nyakanga D.masogora

13. A. takhmisa B. tasdisa C. tathlitha D. tathnia

14. ‘A. kuishauri B. kuwashauri C. kulishauri D.kuyashauri

15. A. ifaayo B.lifaalo C. mfaazo D.yafaavyo

Kutoka swali la I6 mpaka 30, chaguajibu sahihi. 16. Maneno haya hufuatana vipi katika kamusi?

(i) shwari

(ii) sinzia

(iii) sentensi

(iv) staha

A . iii, ii, i, iv

B. ii, iii, i, iv

C. ii, i, iii, iv

D. iii i, ii, iv

17. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.

A. Dalali alikuwa na bidhaa zifuatazo, kabati, meza, viti na rafu.

B. Rita? hujamaliza kazi hiyo nyepesi hivyo!“ C. Wanafunzi wake — Wale waliopata alama za juu zaidi — warnetuzwa leo.

D. Mkulima alipanda nafaka* yaani (wimbi na mlama).

18. Wingi wa sentensi, ‘Karani yulc alimpelekea mkurugenzi waraka huo’, ni:

A. Karani yule aliwapekelea wakurugenzi waraka huo.

B. Makarani Wale waliwapeiekea Wakurugenzi nyaraka hizo.

C. Makarani wale walimpelekea mkurugenzi waraka huo.

D. Karani yule alimpelekea mkurugenzi uyaraka hizo.

19. Chagia kauli ya kutendewa ya sentensi ifuatayo: Menza alikwenda kwa Tumaini akakata kuni.

A. Tumaini alikatiwa kuni na Menza.

B. Tumaini alikatiwa kuni kwa Menza.

20 . Chagua jibu lenye maelezo sahihi.

A. Kefule! ni tamko linalotumiwa kuonyesha kuudhika.

B. Hewala! hutumiwa baada ya kuupata ushindi fulanifi

C. Simile! ni tamko linalotolewa baada ya kumruhusu mtu kupita?

D. Makiwa! hutumiwa ili kurnpa pole mtu aliyepoteza bidhaa zake.

21. neno lipi lenye sauti mwambatano?

A. mvua

B. liwa

C. kunja

D. wayo

22. Kukanusha kwa.) ‘Simba ambao wamejeruhiwa wametibiwa’,ili:

A. Simba ambao wamejeruhiwa hawatatibiwa.

B. Simba ambao hawakujeruhiwa hawatatibiwa.

C. Simba ambao Wamejeruhiwa hawajatibiwa.

D. Simba an-ibao hawakujeruhiwa hawajatibiwa.

23. Chaguajibu lenye maelezo sahihi.

24. Kufisha ni kuviweka vitu hadi viharilbike ilhali kuficha ni kuviondoa vim mahali vinap00nekana_

A. Kisasi ni tendo la kumlipizia mtu kosa alilotenda, na kizazi ni wam wanaoishi katika jamii moja.

B. Zabuni ni zawadi anayopata mtu mashindanoni, na sabuni ni madini yanayotumiwa kusafisha nguo.

C. Kudanda ni kuruka ili kukishika kitu ilhali

D. Kuni zilikatiwa Tumaini kwa Menza.

Kurii zilikatiwa kwa Tumaini na Menza.

25. Ujanja ni kwa sungura ilhali ni kwa kabuzi.

A. kawaida

B. ghafia

C. utulivu

D. msiri

26. Ni jibu lipi lisilolingana na mengine?

A. alamsiki — binuru

B. shikamoo ~ marahaba C. masalkheri — sabalkheri

D. hodi — karibu.

27. Chagua sentensi iliyounganisha sentensi zifuatazo ipasavyo.

A. Nyumba ilikuwa kubwa. Nyumba haikuwatoshea wageni wote.

B . Nyumba ilikuwa kubwa angalau haikuwatoshea wageni wote.

C. Nyumba ilikuwa kubwa madhali haikuwatoshea wageni wote.

D. Licha ya nyumba kuwa kubwa, haikuwatoshea wageni wote.

dada ni ndugu wa kike.

27. Chagua sentensi inayoonyesha hali ya kuagiza.

A. Angetaka angewaimbia.

B. Meza tembe mbili mara moja.

C. Watakaosoma vyema watapita mtihani wao.

D. Uliletewa hilo.

28. Ni sentensi ipi yenye kiambishi ‘ki’ cha ngeli pekee?

A. Mukai alikibeba mgongoni.

B. Shime alienda kijijini.

C. Dola anazungumza akitabasamu.

D. Timau a_kija tutafurahi.

29 Chagua j ibu lenye maneno yasiyoambatanishwa ipasavyo.

A. funguo — kicha

B. nzige ~ wingu

C.hindi — bunzi

D.maji — funda

30 Ni jibu lipi lenye vivumishi pekee?

A. gumu, upesi, nadra, langu

B. safi, yote, sana, halafu

D. Mithili ya nyumba kuwa kubwa, haikuwatoshea Wageni Wote.

nne, kama, mno bora, pengine, zile, kwao

SOma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

J e, umewahi kutafakari kuhusu namna wanafunzi wengi, ukiwemo miongoni mwao, wanavyosafiri kwenda shuleni? Yumkini jibu lako kwa swali hili litadhihirisha kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi hutembea kwenda shuleni, wengine hutumia baiskeli, magari ya umma na ya kibinafsi, pikipiki na garimoshi. Bila shaka aina ya usafiri hutofautiana kulingana na uwezo wa kiuchumi na umbali baina ya nyumbani kwa mwanafunzi na shule yake.

Kila aina ya usafiri ina changamoto maalum. Mathalani ikiwa umezungumza na wenzako ambao hutembea kwenda shuleni, haikosi wamekuelezea dhild wanazokumbana nazo. Licha ya safari za aina hii kuwachosha wanafunzi, ni wazi kuwa Wanafunzi wengine hata hukosa masomo kwa sababu ya kutopitika kwa njia wakati wa mvua nyingi. Pengine hata wewe umewahi kujipata katika njia panda baada ya daraja unalovukia kusombwa na maji ya rnto uliofurika. Isitoshe, watembeao huweza kuathirika kiafya wakati wa kipupwe. Baridi huweza kuwasababishia pumu au hata kichomi. Wengine huwa katika hatari ya kuteleza kwenye njia zenye matope na kuvunjika viungo vya mwili. Hawa pia wamo katika hatari zaidi ya kutekwa nyara na hata kunyanyaswa kimapenzi.

Wanafunzi Wengine huwaliusudu Wale ambao husafiri shuleni, ama kwa gari la shule, au la kibinafsi. Wakiulizwa kuhusu kiini cha husuda hii, wanaserna kwamba Wenzao hawa hawachoki kwani magari haya yanawachukua kutoka rnalangoni mwa nyumba zao. Hate. hivyo, ukichunguza vyema utapata kwamba hata hawa wana matatizo sugu. Kwa vile magari ya shule huwabeba wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali, magari haya hayana budi kuanza safari mapema. Hili huwalazimu wanafunzi nao kuamka alfajiri na mapema ili kuyawahi magari haya. Matokeo ni kwamba Wanafunzi wengi hawadiriki kulala usingizi wa kutosha. Kuna wale ambao hulala saa nne usiku baada ya kukamilisha kazi za darasani, kisha wanaraushwa saa kumi ili kujitayarishia basi la saa kumi na rnoja. Wanafunzi wa aina hii hukumbwa na uchovu, na bila shaka husinzia darasani.

Isitoshe, wanafunzi wanaotumia usafiri wa umma hulalamikia msongamano wa magari ambao unawafanya kukawia njiani, na hata kupewa adhabu kwa kuchelewa kufika shuleni. Wengine hata hukataliwa na magari ya abiria, eti wanalipa fedha kidogo, na kuwasababishia Wenye magari hasara. Wanafunzi hawa huaibika na kulazimika kutembea hadi shuleni. Hali kadhalika, magari ya umma humpa mwanafunzi mazingira ya kujifunzia tabia; nzuri na mbaya. Pamoja na Wanafunzi hawa kupata fursa ya kutangamana na wenzao kutoka shule nyingine, wao pia huweza kuathiriwa vibaya na hulka za wasafari wengine. Kuna Wale ambao huiga lugha, mitindo ya mavazi, namna ya kutembea, na hata mienendo mingine ya madereva na utingo. Wengine huishia kuwa waraibu sugu Wa vileo kutokana na vielelezo wanavyopata kwenye magari haya. Muziki, picha za video, na mazungumzo kupitia vyombo vya habari vilivyo kwenye magari haya huchangia kuzorotesha tabia ya wanafunzi. Hii ni kwa sababu baadhi ya masuala yanayozungumziwa ni ya aibu na hayapaswi kusikilizwa na watu wa umri mbichi.

Ni dhahiri kwamba kila aina ya usafiri ina athari zake, Hata hivyo, Baniani mbaya kiatu chake dawa. Usafiri unahitajika katika kufanikisha masorno ya Wanafunzi, na katika uchukuzi wa bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanahitaj i shuleni. Ni j ukumu la kila mwanajamii kuhakikisha kwamba mikakati ifaayo imewekwa ili kukinga dhidi ya madhara yanayoandamana na kila aina ya usafiri. Wanafunzi nao wakae ange kutambua watu ambao huenda wakawatosa katika maovu. Wachuje ya kuiga na ya kukataa. 31. Kulingana na aya ya kwanza:

A. Wanafunzi wengi huabiri vyombo vya usafiri ili kufika shuleni.

B. Anayeencla kwa kawaida huwazia njia yake ya usafiri.

C. Utfiuzi wa njia ya usafiri hutegemea masafa kati ya anakoishi mwanafunzi na anakosomea.

D. Wale walio na pesa kidogo hulazimika kutumia magari ya umma na baiskeli.

32. Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu.

A. Matatizo ya usafiri hutofautiana kulingana na aina ya usafiri.

B. Barabara mbaya huweza kualhiri utendaji wa wanafunzi kjelimu.

C. Mwandishi ana hakika kwamba msomaji ameambiwa yanayowapata wenzake.

D. Magonjwa mengine huweza kutokana na hali ya anga.

33. Chagua madhara ya aina ya usafiri unaozungumziwa katika aya ya pili. A A. mvua nyingi, kutatizika kirnawazo

B. kupatwa na ajali, kuchukuliwa kwa nguvu

C. Kuharibika kwa daraja, majira ya baridi

D. ulemavu mwilini, kuingiliana na mazingira yasiyovutia.

34. Aya ya tatu imebainisha kwamba wanafimzi wengine:

A wangetaka aina ya usafiri imaohusu nyumbani kwao

B Wanadhani kwamba wanaosafiri kwa magari hawasumbuki

C wanapenda hali ya usafiri usiomhitaji mtu kutumia nguvu

D wanaona kwamba Wanaomiliki magari huwa na matatizo mepesi.

35. Ni jibu lipi sahihi kulingana na aya ya tatu?

A. Kutumia gari moja kusafina humnyima mwanafunzi mapumziko yafaayo.

B. Magari yakianza safari shuleni mapema huwafanya wanafimzi kumaliza kazi mapema.

C. Wanafunzi wakichoka hushindwa kuona umuhimu wa masomo darasani.

D. Kupitia sehemu mbalimbali za gari humfanya mwanafunzi kuraushwa.

37. Kulingana na aya ya nne:

A. Usafiri wa umma huwafanya wanafunzi kulaumiana. B. Wanafunzi wengi hawafurahishwi na hali ya rnagari kuchelewa nyumbani. C. Msongamano wa magari huweza kuathiri utulivu wa wanafunzi shuleni. D. Wanafunzi hupuuzwa garini na waliokosa nauli. 38. Maana ya methali, “Hakuna masika yasiyokuwa na mbu” imejitokeza katika kifungu kwani magari ya umma: A. huwaletea wenye magari hasara, huonyesha mienendo rnizuri

B. hushusha hadhi ya wanafunzi, huonyesha namna ya kuwasiliana

C. hukuza ushirikiano Wa kijamii, hupalilia kuzorota kwa maadili

D. huwaongezea wanafunzi maarifa, huharibu namna ya kujipamba.

38 Aya ya nne imebainisha kwamba

A. Wale Wanaokuwa waraibu zaidi ni wale ambao Wanaingiliana sana na madereva.

B. J insi mtu anavyolembea hulingana na tabia zinazosababishwa na mienendo ya utingo.

C. Mazungumzo kwcnye magari ya abiria yanataka kumjengea mwanafunzi hali yenye vielelezo vyema kwao shuleni.

D. Hulka ya mwanafunzi huweza kuathirika vibaya anapopata maarifa yasiyolingana na mahitaji ya rika lake.

39 Mtazamo Wa mwandishi katika aya ya mwishb ni kwamba:

A. Wanafunzi wakiwa makini wanaweza kujiepusha na madhara ya usafiri.

B. Wasafiri wakijua hasara za safari wataimarisha juhudi za kusoma.

C. Wanajamii wakitumia njia zifaazo shule zitapata vifaa vinavyohitajika.

D. Watu wakizifahamu tofauti za usafiri watapimguza maovu kwa wasomao.

40 Maana ya ‘huwahusudu’ kulingana na kifungu ni:

A. huwapenda kwa hali yao

B. huvutiwa na hali yao

C. huwafikiria kwa hali yao

D. huhimizwa na hali yao.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Simba na fisi walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana. Urafiki Wao ulishinda hata uhusiano wa ndugu wa toka nitoke. Ulikuwa ule uhusiano wa, mmoja anapojikwaa dole, anayeuhisi uchungu hasa ni huyo rafikiye. Wenzao porini hawakuisha kuusifu urafiki huu. Hakika hata waliwahimiza watoto wao kuiga mfano wa simba na fisi. Kilichowavutia Wanyama zaidi ni hulka ya simba na fisi kuchuma pamoja na kuzikimu familia zao pamoja.

Hali iliendelea hivyo hadi Wakati simba na fisi walipojifungua vitinda mimba wao. Uzazi huu ulisababisha mabadiliko makubwa katika maisha yao. Licha ya uzee uliokuwa umebisha hodi, simba na fisi walikuwa na vinywa Zaidi vya kulisha. Kadhalika, vitoto hivi vikembe vilihitaji uangalizi zaidi, havingeweza kuachiwa ndugu zao. Hali hii iliwafanya wasiweze kuandamana usasini. Waliafikiana kupishana zamu katika majukumu yao. Wakati ambapo simba angeenda kuwinda, fisi angebaki nyumbani akiwatunza watoto. Zipo baadhi ya nyakati, japo kwa nadra nmo, fisi alipojitolea kwenda kuwinda. Jambo lililomtia simba Wahaka ni kwamba kila fisi alipobakia nyumbani, chakula walichokuwa wamekihifadhi kwa matumizi ya baadaye kiliota mbawa.

Fisi alipoulizwa hakukosa kauli ya kujitetea. “Mambo yamekuwa magumu siku hizi. Ulezi una changamoto zake. Kumbuka pia tuna waivu. Kozi amekuja hapa na kutaka kuwanyakua watoto wetu. llibidi nipambane kwa jino na ukucha kuwaokoa. Katika hali hii nilisahau kuwa ghala lilikuwa wazi. Hata kitali kilipokwisha, nilitahamaki kuwa ghala lilikuwa tupu, ikawa ni yale ya mwangaza mbili…,” akasema fisi. Lile ambalo simba hakujua ni kwamba fisi alikuwa akikiiba chakula kujinufaisha yeye na Wazazi wake.

Tabia hii ya fisi iligeuka kuwa ngozi ya mwili‘ Simba naye alizidi kumshuku fisi. Hata hivyo, alipoendelea kuuliza kuhusu muujiza wa kutoweka kwa chakula, fisi alimlaghai kwamba kwa kweli chakula kilikuwa kikichukuliwa na simba jike mwingine aliyekuwa akiishi ziwani. Hili lilimchcmsha simba roho, akakata shauri kwenda moja kwa moja kukabiliana na hasidi huyo. Simba alisimama ukingoni mwa ziwa huku akiyatazama maji yaliyotulia kana kwamba yanamwogopa. Mbele yake, ndani ya maji, alirnwona simba jike mwenzake aliyefanana naye karna shilingi kwa ya pili. “Kumbe ni kweli kuwa dada yangu huyu hutuendea kinyume? Kumbe huyu ndiye anayetaka kuutia ufa udugu baina yangu na fisi?” simba alijiuliza.

Simba hakujua vipi, lakini alijipata ndani ya ziwa; hasira imemtuma kupambana na simba jike mwenzake. Alitwaa mafumba yake kumchanachana huyo simba, lakini lo! Alijipata anakipiga kivuli chake pambaja majini. Haukupita muda mrefu kabla ya simba kuhisi mng’at0 mkali kwenye mguu wake.

Alipotazama alimwona mamba mkubwa ajabu anaendelea kung’wafua minofix ya nyama kutoka pajani mwake. Alitaka lmtoa ukemi lakini akajiasa. “Simba haonyeshi maumivu hata mbele ya matatizo makubwa. Huku kutakuwa kujidhalilisha,” simba alijisemea. Baadaye alimrukia mamba kwa hamasa kuu, moto wa mapigano ukawaka. Mapambano yalipokatika, wawili hawa walikuwa wamehasirika si haba. Simba alikuwa arnedhoofika mguu, naye mamba akabaki na kigutu cha rnkia. Simba alifika nyumbani akiwa hoi kwa maumivu, maj onzi na kukatika tamaa. Fisi alipomtazama, michirizi ya machozi ya mamba ilimtiririka kama maji bombani. Alimwendea simba na kutaka kumkumbatia. Hata hivyo, mtazamo wa macho ya simba ulimwonya fisi dhidi ya tendo hili na kumfahamisha fisi kuwa urafiki wao wa miaka na mikaka urnefikia ukingoni.

41. Simba na fisi walikuwa marafiki wakubwa kwani:

A. Wote waliwashinda ndugu zao katika kujali urafiki. B. Kila mmoja aliathiriwa na malatizo ya mwenzake.

C. I-Iali yao ya kutegemeana iliigwa na wengi.

D. Walikuwa pamoja Wakati familia zao zilikuwa zikijikimu.

42. Kulingana na aya ya pili:

A. Uzazi uliwadhuofisha waliokuwa marafiki wa fisi na simba.

B. Kupata vitinda rnimba kuliwasababishia fisi na simba kuzeeka.

C. Jukumu la kulea liliwafanya simba na fisi kuwa makini zaidi.

D. Kuwa na vikembe kulipunguza muda wa fisi na simba kuwa pamoja.

43. Ni dhahjri kwamba:

A. Ndugu hawajui kuwalinda wadogo wao.

B. Kuwa na wawto wengi kuliwafanya fisi na simba kufanya kazi kwa mpango.

C. Haikuwa kawaida ya fisi kuwinda.

D. Ongezeko la majukumu Iilipunguza juhudi

za fisi na simba kuzitafutia familia.

44. Chagua tabia za fisi kwa mujibu wa aya ya tatu.

A. mwenye ubinafsi, asiyekubali makosa yake»

B. anayejua mustakabali wake, mdanganyifu

c. mwenye kufahamu mazingira yake, jasiri

d. anayetafuta ubingwa, asiyeaminika kwao.

45. Ni jibu lipi sahihi kulingana na kifimgu?

A. Malezi ya fisi na simba yamehimji hali isiyo na vikwazo vya maadui.

B. Utetezi wa fisi umefanya simba kutojua manufaa ya wazazi wa fisi.

C. Simba na fisi wamebuni njia ifaayo ya kuyaboresha maisha yao.

D. Kutoshughulikia jambo pamoja kumefanya familia ya fisi na simba kutojimsheleza kwa chakula.

46. “Tabia hii ya fisi iligeuka kuwa ngozi ya mwili”, ina maana kuwa:

A. Ilikuwa hulka ya fisi kumsingizia yule simba jike.

B. Kuiba chakula kwa fisi kulikuwa mazoea.

C. Hali ya wengine kushuku nyendo za fisi iliongezeka.

D. Uzembe wa fisi uliendeleza kutoshiriki kazini.

47“Kumhe ni kweli kuwa dada yangu huyu hutuendea kinyume?” inaonyesha kuwa simba:

A. amehuzunishwa na usaliti unaosababishwa na udugu

B. anasikitika kwamba urafiki kati ya ndugu ulikuwa unaharibika

C. amehakikisha kwenye fikra zake kuwa anajuta kumgombeza fisi

D. anathibitisha mawazoni kuwa fisi hana hatia.’

48. Simba hakupiga kelele alipoumwa kwa sababu:

A. alitaka kuonyesha kuwa kuna Wengine wajanja kuliko mamba

B. alitarajia kuamini kwamb”a hapati maumivu kwa mamba _ _

C. alitaka kuihifadhi hadhi yake ya kawaida

D. aliazimia kumshambulia adui kwa hasira.

49. Kauli, ‘ilimtiririka kama maji bombani’ imetumia tamathali gani ya usemi?

A. tashbihi

B. sitiari~

C. nahau

D. kinaya

50 .Kulingana na kifungu, maana ya ‘kuutia ufa’, ni:

A. kuudharau

B. kuudhoofisha

C. kuuvunja\

D. kuukosoa.

2015 KCPE Kiswahili Past Paper-Marking Scheme/Answers

1.C 2.B 3.C 4.C 5.A 6.B 7.B 8.C 9.B 10.B 11.D 12.D 13.A 14.C 15.A 16.D 17.C 18.B 19.D 20. D 21.C 22.C 23. A 24.C 25.C 26.B 27.B 28.A 29.C 30.D 31.C 32.C 33.B 34.B 35.A 36.C 37.C 38.D 39.A 40.B 41.D 42.D 43.C 44.A 45.D 46.B 47.D 48.C 49.A 50.B