2019 KCSE Kiswahili Karatasi ya 2 Past Paper
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Kijiji chetu kilikuwa kimeanza kuingiwa na wasiwasi. Katika kipindi cha miaka michache iliyopita tulikuwa tumewapoteza watu kadha na hakuna aliyeelewa kiini hasa cha majanga haya.
Wazee walisikika wakisemezana kwa sauti za chini.
Hatukujua hasa walichosema lakini ilikuwa bayana kuwa kijui chetu kilikuwa juu ya mchongoma.
Kuumi kwetu kuna mambo yatokeayo yakaonekana miujiza.
Tunabaki kutapatapa kuelezea chanzo shake na wesemavyo, akili ni nywele kila mtu ana zake.
Ila zipo nywele za koto na za singa.
Lakini kuna watu wenye kuandamwa na tata, mti wowote uliokuwa karibu ulishikiliwa kwa tumaini la kuleta nafuu.
Ndiyo, nafuu.
Na ndivyo ilivyotokea kiasi cha kila mtu kuwa bingwa wa kufasiri asili ya janga na suluhu yake.
Hali hii iliendelea mpaka walipofika wataalamu kuuini kwetu na kufanya utafiti wa kisayansi uliotufumbulia asili ya dhiki zetu.
Siku hiyo ya kutolewa matokeo ya utafiti, kuul kizima kilijumuika kwenye uwanja wa shule mapema.
Hakuna aliyeonyesha use wa furaha.
Ilikuwa kama tuliokuwa mahakamani tunasubiri hukumu ya kesi ya jinai dhidi yetu.
Siyakumbuki yote aliyosema yule mtaalamu lakini yapo yaliyotugusa sote.
“Najua mna hamu ya kujua tatizo liko wapi.
Kabla ya kulieleza tatizo lenyewe ningependa kusema poleni kwa misiba iliyowaandama.
Kuwapoteza wapendwa si pigo kwa familia tu, bali pia kwa kuui na taifa.
Na kuanzia sasa ninawaomba tushirikiane kuibadilisha hali hii.
Hatuwezi kuendelea kuishi hivi,” alisema huku wanakuui wanamtazama kwa masikitiko makubwa. “Binadamu yumo katika awamu ya kujiangamiza”,aliendelea, “amefanya uvumbuzi wa teknolojia aali lakini ambayo sawa na mwaridi, ina miba.
Miba hii sasa inamchoma kila aitundaye teknolojia. Kwa sababu ya wingi wetu, sasa tunataka kuzalisha mazao yetu haraka.
Kwa sababu ya ongezeko kubwa la idadi ya watu walaji ni wengi lakini ardhi inazidi kujibana. Njia ya pekee ya kuongeza lishe ni kupitia uzalishaji zaidi wa vyakula. Katika ulimwengu ambapo vipando vile vile hurudiwa kupandwa kwenye ardhi ile ile, pato lake hupungua. Jibu la kuinua pato ni teknolojia.
Teknolojia hii imebuni uzalishaji wa mbolea ya kemikali ambazo huchochea rotuba kwenye ardhi. Urutubishaji wa ardhi yetu ndogo umetuwezesha lcuzalisha chai, kahawa, mahindi na mazao mengine kwa wingi ili kukidhi haja yetu ya chakula.
Zamani ardhi ilipokuwa kubwa na idadi ya watu ikawa ndogo, haja hii ya mbolea haikuwepo. Ardhi iliachwa kujirutubisha yenyewe. Madhara tuyaonayo sasa hayakuwepo wakati huo.” “Leo hii utashi wetu wa lcujitosheleza umetusukumizia ukingoni mwa maisha.
Vyakula vyetu sasa vina kemikali hatari kutokana na mizizi ya mimea kufyonza virutubisho vyenye nitrojeni.
Virutubisho hivi hustawisha mimea. Hata hivyo mimea hii tunayoila ina kemikali hatari kwa miili yetu. Kemikali hizi vilevile huingia kwenye nyasi ambazo huliwa na mifugo wetu. Mifugo hao hudhurika, nasi tunapofaidi bidhaa zao tunadhurika. Hata mito yetu na visima hupokea mikusanyiko ya kemikali hizi hatari, nasi tunazinywa kupitia kwa maji.
Kemikali hizi husababisha saratani, na hili ndilo tatizo la kuut hiki.” Kauli hii ya mwisho iliutikisa umati ule. Sauti za wanaktjui zilisikika zikinong’onezana.
Wengi wa wanakuut waliona kama kila kite pale kuutnt kilikuwa chanzo cha adhabu ya kifo kwao. Baada ya kule kutanabahishwa, ilisikika sauti ya mlevi mmoja aliyesema kwa sauti kubwa kabisa, “Ni hivi, ama tule hivyo vibaya tufe polepole au tuache kuvila tufe mara moja.” Tamko hili la mlevi liliwasisimua wote waliokuwa pale, wakapata walau sababu ya kucheka.
Kucheka huku kuliwatia watu matumaini, wakaanza kuuliza maswali. Kwa nini mbolea itengenezwe kutokana na kemikali hatari? Hivi dunia haijui kuwa ipo hatari kwenye mbolea hizo? Je, waache kunywa maji na kutupa vyakula walivyokuwa navyo? Waliuliza maswali haya na mengine mengi.
Yule mtaalamu hakuwa na mengi ya kusema kwa sababu alifahamu kuwa kila aina ya teknolojia ina faida na madhara yake. Kwa hivyo alieleza kwa ufupi.
“Kemikali hizo ndizo huchochea rutuba ya ardhi ambayo huiwezesha mimea kukua na kutupa mazao mcnbi.
Dunia inafahamu fika madhara ya kemikali zinazotumiwa kwenye mbolea lakini ifanyeje? Watu watakao kulishwa ni wengi.
Ardhi imepungua kwa sababu ya wingi wa watu. watu wanataka kula ilhali ardhi hiyo ndogo haina tena rutuba.
Hata maji hayo yaliyoathirika mtayanywa tu bado.
Mtaishije bila maji Mtapika vipi? Mtakunywa nini? Hali hii tunaweza kuiondoa polepole kwa kuwekeza kwsnye ufugaji wa kuku, ng’ornbe na mbuzi wengi ili tutumie mbolea yao kurutubisha ardhi yetu. Wanasayansi wanasema itachukua yapata miaka mitano kuirejesha ardhi katika hali yake asilia.”
Maelezo ya mtaalamu yule yalilta nafuu ya namna fulani kwa wanakijiji. Mzee mmoja alipewa nafasi kuzungumuza kabla ya kikao kufungwa.
Mkutano ulipomalizika kijiji kilijua tatizo lilipokuwa na kuumaliza uvumi uliokuwa unaoteshwa kila leo.
(a) Eleza sababu mbili za wanakijiji kuuona ugonjwa uliozuka kuwa miujiza.(alama 2)
(b) Eleza madhara manne ya kemikali za mbolea kulingana na kifungu. (alama 4)
(c) Bainisha mambo matatu yanayochochea kubuniwa kwa teknolojia mpya kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
(d) Andika mambo mawili yanayoonyesha kuwa wazee wa jamii hii walikuwa na hadhi.(alama 2)
(e) Fafanua maana ya ‘nywele za koto’ na ‘nywele za singa’ kwa kurejelea kifungu hiki (alama 2)
(f) Kipe kifungu hiki anwani mwafaka (alama 2)
2. UFUPISHO (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Demokrasia ya uwakilishi huweza kujitokeza kwa namııa tofautitofauti kutegeıvca ır‹atakwa ya nchi mahususi. Demokrasia ya Urais ni aina mojawapo ya demoloasia ya uwakilishi. Aina hii ya demokrasia humpa rais mamlaka makuu juu ya serikali.
Rais huchaguliwa ama kwa njia ya rnojiı t.wa moja, au kwa kutumia wawakilishi. Yeye hawi tu kiongozi wa taifa, bali pia wa serikali kaına iliivyo Kenya, Marekani na Ajentina. Hali kadhalika, kuna Demokrasia ya Bunge.
Aina hii huipa bunge mamlaka makubwa.
Kitengo cha utekelezi cha serikali hupata mamlaka yake katika bungeni. Kiongozi wa taifa na kiongozi wa serikali huwa watu tofauti na wenye viwango tofauti vya mamlaka. Kwa kawaida, kiongozi wa serikali huwa na mamlaka makubwa zaidİ kama ilivyo Uingereza. Demokrasia ya kimabavu huelekea kupingana na dhana halisi ya deınokrasia.
Katikaa
demokrasia hii tabaka la juu pekee ndilo lenye haki ya kuchagua wawakilishİ Wa taifa. Umma lıauna lıaki hiyo. Mfano wa demokrasia hii ni Urusi.
Demokrasia ina manufaa mengi. Demokrasia hulinda masilahi ya wananchi wote; si walio wengi, si walio wachache, si wenye nguvu, si wanyonge…Demokrasia pia husaidia kugatua mamlaka, lıivyo kuzuia kundi dogo kuwa mamlakani daima.
Hili hufanikishwa na chaguzi za mara kwa mara. Kwa vile sheria haibagui, demokrasia basi hukuza usawa kwa wote. Wale wanaochaguliwa hujaribu kuweka sera mwafaka kwa kuwa hawadumu mamlakani. Kuhusishwa kwa umma katika kuamua watakaowatawala na kuwepo kwa kipındi mahususi cha kuhudumu hupunguza uwezekano wa kutokea kwa mapinduzi.
Hali kadhalika, demokrasia huchochea mabadiliko katıka nchi kwa kuwa kila utawala huwa na kipindi chake maalumu ambapo umma hupata nafasi ya kuubadilisha, na hivyo kubadili sera na rnwelekeo wa nchi.
Demokrasîa huipa umma nafasi ya kujifunza mambo mengi kuhusu siasa.
Wakati wa uchaguzi, wagombeaji hunadi sera na rawaza zao, na hivyo kuelimisha umma. Demokrasia pia huwafanya watawala kuwa na tahadhari na kuwajibika kwa kuwa umma ulioerevuka kisiasa unawatia kwenye mizani na huenda usiwachague tena.
Ni dhahiri kwamba demokrasia ina dhima kuu katika maendeleo ya nchi. Hivyo ipo haja ya kuthamini na kuendeleza mifumo ifaayo ya kidemokrasia ili kuhakikisha kwamba hak i ya ki la raia imelindwa.
(a) Fupisha ujumbe wa aya tano za kwanza kwa maneno 110. (alama 10; 1 ya mtiririko)
Matayarisho
————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— —————————————————————————
Nakala Safi
————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— —————————————————————————
(b) Kwa maneno 50, eleza masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (alama 5; 1 ya mtiririko)
Matayarisho
————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— —————————————————————————
Nakala Safi
————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— ————————————————————————— —————————————————————————
3. Matumizi ya Lugha: (Alama 40)
(a) Andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)
(i) irabu, konsoızanti, konsonartti irabu, konsonanti , irabu
(ii) konsonanti, konsonanti, irabtı, irabu
(b) Ainisha mofimu katika maneno yafuaatayo: (alama 2)
(i) asemavyo
(ii) mwangwi
(c) Onyesha aina za nomino katika sentensi ifuatayo.(alama 3)
Shule nzima ilifurahia ukarimu wa Shirika la Tugawane.
——————————————————
——————————————————
(d) Andika sentensi ifuatayo katika wingi (alama 1)
Seremala aliulainisha ubao huo ili kutengeneza kasha amuuzie mlinzi huyo.
————————————————————————-
(e) Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo:
(i) Nafasi katika orodha (alama 1)
———————————————
(ii) Kutobagua (alama 1)
———————————————–
(f) Andika sentensi ifuayavyo katika hali ya ukubwa (alama 1)
Mtu huyo alifuata njia iliyomwelekeza mjini
———————————————————————
(g) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo bila kupoteza maana.
(i) Mhadisi alikarabati mtambo.
Mtambo ulikuwa kiwandani.
(Unganisha kuwa sentensi moja bila kutumia kiunganishi.)(alama 1)
(ii) Kembo alishona fulana hiyo vizuri sana. (Tumia kielezi cha kiasi badala ya vile Yilivyopigiwa mstari.) (alama 1)
(h) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 2)
Mkurugenzi alisema kwamba wangetoa nyongeza ya mshahara mwaka ambao ungefuata.
(i) Geuza sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timiIifu.(alama 1)
Ni wazi kwamba gharama ya maisha itapanda bei ya mafuta ikipanda.
(j) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi. (alama 1)
Badi huwa hapitii hapa, huenda usimpate.
(k) Zuri ni kwa baya, aminifu ni kwa ……………….. na vivu ni kwa …………..- (alama 2)
(l) Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (alama 2)
(i) sukari …………………………………………..
(ii) Teo ……………………………………………..
(m) Changanua sentensi ifuotayo kwa kielelezo Cha mistari (alama 2)
Mvua inseptısa na ıvatu wameanza kuondoka. ——————————————————————
——————————————————————–
(n) Vyakula viliandaliwa. Vyakula vilikuwa na viinilisha muhimu
(Unganisha kuunda sentensi changamano.)
(o) Bainisha yambwa na chagizo katika sentcnsi ifuatayo. (alama 3)
Zumari aliıntunzia Keto watoto hao kwa upendo. —————————————————————–
——————————————————————-
(p) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mnwili ya kiambishi ‘ku’.
(q) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo.
Usalama ukiimarishwa watalii wengi watakuwa wanazuru humu.
(r) Unaporidhika na jambo unasema hewala, unaposhangilia timu yako kwa kupata ushindi unasema …………… na unapotaka usikivu unasema ……………….(alama 2)
(s) Jepesi ni kwa rahisi, ukuta ni kwa ………………….. na njia ni kwa ……… ………….. (alama 2)
(t) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya dua na tua.(alama 2)
(u) Mzee tuma ni mraibu wa vileo .
Baada ya muda watoto wake wawili wanakuwa watumizi sugu wa vileo inayoweza kutumiwa kuelezea hali hii. (alama 1) ———————————————————————
(v) Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha uteuzi.(alama 2)
(d) ISIMUJAMII: (Alama 10)
Wewe ni mhubiri katika Maabadi ya Shamu.
Umealikwa kuwahubiria wanafunzi wa Shule ya Upili ya Lulu.
Fafanua sifa kumi za lugha utakayotumia.
2019 KCSE Kiswahili Karatasi ya 2 Past Paper-Marking Scheme/Answers
1. UFAHAMU
(a) (i) Walikuwa hawaujui.
( ) Watu wengi walifariki. 2 x 1 = 2
(b) Madhara ya kemikali ya mbolea
(i) Hudhuru afya za watu/husababisha magonjwa/ husababisha kansa/saratani
(ii) Huwadhuru wanyama/ mifugo
(iii) Hutia sumu kwenye mimea.
(iv) Huchafua visima na mito.
(v) Husababisha vifo vya watu na mifugo. 4 x 1 = 4
(c) Mambo yanayochochea teknolojia mpya kubuniwa:
(İ) Kupungua kwa mashamba/ ardhi inazidi kujibana
(ii) Kuzorota kwa rutuba na kupunguza uzalishaji/ vipando hurudiwa.
(iii) Ongezeko la watu watakao lishe/ wingi wa watu.
(iv) Kutoipa ardhi nafasi ya kupumua na kujirutubisha. 3 x 1 = 3
(d) Wazee wana hadhi kwa sababu.
(i) Jamii inataka kujua wanachokifikiria kuhusu janga/ jamii inatambua mchango wao katika usuluhishaji wa changamoto..
(ii) Mzee mmoja anapewa nafasi kuhitimisha kikao. 2 a 1 = 2
(e) ‘Nywele za koto inarejelea wenye mawazo finyu au ya kubabaisha na ‘nywele za singa’ inarejelea wenye mawazo ya kina/mapevu. / Kila mtu ana uelewa wake; Viwango vya uelewa havifanani. 1 x 2 = 2
(f) Anwani Mwafaka kwa kifungu.
(i) Madhara ya mbolea
(ii) Hofu kijijini
(iiİ) Janga la saratani/ Saratani
(iv) Madhara ya teknolojia 1 x 2 = 2
2. UFUPISHO
(a)Demokrasia ni mfumo wa utawala wa kuwachagua wawakilishi moja kwa moja. Demokrasia ni utawala wa umma.
(iii) Umma huhakikishiwa haki fulani za kimsingi ambazo haziwezi kukiukwa. (iv) Haki hizo hutambuliwa na kudhibitiwa kimataifa.
(v) Demokrasia hushirikisha uchaguzi ulio huru na wenye haki.
(vi) Huwezesha kuhusika kikamilifu kwa umma katika siasa na masuala mengine ya kijamii.
(vii) Husisitiza kulindwa kwa haki za kibinadamu na za wananchi.
(viii) Huwa ni utawala wenye usawa wa kisheria/ ni utawala ambao huongozwa na sheria.
(ix) Kila nchi hufasiri dhana ya demokrasia kwa namna inayoifaa yenyewe.
(x) Kuna demokrasia ya moja kwa moja: raia hupigia sera fulani kura bila kupitia kwa wajumbe.
(xi) Kuna demokrasia ya uwakilishi — demokrasia ya uwakilishi ya urais, demokrasia ya uwakilishi ya bunge na demokrasia ya uwakilishi ya kimabavu.
(b) (i) Demokrasia hulinda maslahi ya raia wote.
(ii) Hugatua mamlaka na kuzuia kundi dogo kudumu mamlakani.
(iii) Hukuza usawa kwa wote kwa kuwa sheria haibagui.
(iv) Wanaochaguliwa huweka sera mwafaka.
(v) Kuhusishwa kwa raia hupunguza uwezekano wa kutokea mapinduzi.
(vi) Hukuza mabadiliko kwa kuwa uongozi huwa na kipindi maalumu cha kuhudumu.
(vii) Demokrasia hufunza watu kuhusu siasa hasa wakati wa kampeni.
(viii) Watawala huwa na tahadhari na kuwajibika.
(ix) Demokrasia ina dhima muhimu kwa nchi hivyo inafaa kuendelezwa.
3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
(a) (i) Ondoka, ongoka, anguka, atwaza
(ii) Ndoa, ngao, mbao, twaa
(b) (i) a – nafsi ya tatu/mtenda/ ngeli/ kiambishi cha umoja/ kiambishi cha kiima sem- mzizi.
a – kauli tenda/ kiishio/ kimalizio vyo – kirejeshi/namna
(ii) mw — umoja angwi — mzizi
(c) Shule – nomino ya jamii/ makundi / ya kawaida ukarimu. nomino dhahania Shirika la Tugawane — nomino ya pekee 3 x 1 = 3
(d) Maseremala walizilainisha mbao hizo ili kutengeneza makasha wawauzie walinzi hao.
(e) (i) Mungla alikuwa wa kwanza katika mbio hizo.
(ii) Kuli yeyote anaweza kupakia mizigo hiyo chomboni.
(f) Jitu hilo lilifuata jia/ jijia lililolielekeza jijini.
(g) (i) (i)Mhandisi alikarabatia mtambo kiwandani.
Au (ii) Mtambo ulikarabatiwa kiwandani na mhandisi.
Au (iii) Kiwandani kulikarabatiwa /mlikarabatiwa/palikarabatiwa mtambo na mhandisi. Au Mtambo uliokuwa/ ambao ulikuwa kiwandani ulikarabatiwa na mhandisi.
(ii) Kembo alishona fulana hiyo tena. Au Kembo alishona fulana hiyo mara nyingi/maradufu/daima/maranyingine.
(h) (i) “Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema. Au (ii) “Watatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema.
Au (iii) “Mtatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema.
Au (iv) Mkurugenzi: Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao.
(i) (i) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda baada ya kupanda kwa bei ya mafuta. Au
(ii) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta. Au
(iii) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ingekuwa imepanda iwapo bei ya mafuta ingekuwa imepanda. Au
(iv) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda bei ya mafuta ilipopanda.
(j) Badi huwa anapitia (hupitia) hapa, huenda ukampata/ umpate/utampata.
(k) aminifu — saliti 1/ 0 vivu — kakamavu/ shupavu
(i) (i) sukari I-I, I-ZI( aina nyingi)
(ii) teo U — ZI
Mvua imepusa na watu wameanza kundoka. KN (N) KT(T) U
KN(N) KT(T+S T)
Au S /+ U+S2
Si KN+KT
N
N Mvua
KT T
T imepusa
U na
S2 KN+KT
N
N watu
KT Ts T
Ts wameanza
T kuondoka
KN (N) KT(T) U+KN(N)+KT(Ts+T)
(n) (i)Vyakula vilivyokuwa na viinilishe muhimu viliandaliwa.
Au (ii) Vyakula vilivyoandaliwa vilikuwa na viinilishe muhimu.
Au (iii) vyakula ambavyo viliandaliwa vilikuwa na vinilishe muhimu. 2
(o) Keto — yambwa tendewa / kitondo watoto hao — yambwa tendwa /kipozi kwa upendo-Chagizo.
(p) (i)Ku-nafsi ya pili umoja Baba anakupenda.
(ii)Mahali/ ngeli ya mahali/ mahali kusikodhihirika — Huku kwao kunapendaza. Kitenzi jina/ ngeli ya kitenzi-jina — kucheza kule kunavutia.
(iii)Wakati uliopita/ wakati uliopita hali ya kukanusha— wageni hawakufika mapema.
(r)hoyee!/ huree!/hario!/ oyee!
(s)jamani!/jama! enyi!/nyungwa!/ aisee! 1/ 0 ukuta — kiambaza/ kizuizi/ kizingiti/ngome/boma
1/ 0 njia — baraste/namna/mbinu/mtindo/ jinsi/ sampuli
(t) dua — ombi
tua — sita, pumzika, tulia, aibu, weka mzigo chini. Tanbihi: Sentensi sharti ibainishe maana hizi.
Mfano:
Msafiri alitua mzigo akapiga magoti na kumpigia Mola dua.
(u) (i)Mti rnkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
Au (ii) Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina.
Au (iii) Samaki huanza kuozea kichwani.
(v) (i) Doto hakula wala kunywa kwa siku kadha.
(ii) Je, utakula wali au sima?
(iii) Anna usome kwa bidii au ufeli mtihani wako.
4 ISIMUJAMII (Alama 10)
(i) Msamiati wa kidini/ matumizi ya msamiati teule wa kidini.
(ii) Lugha ya kuwashawishi kumtii Mungu.
(iii) Kurejelea vifungu vya vitabu vitakatifu.
(iv) Kuchanganya ndimi/ kubadili msimbo.
(v) Lugha inaweza kuwa rasmi au isiyo rasmi.
(vi) Lugha yenye toni kali ya kuonya.
(vii) Kuwasawiri kama viumbe ambao ni wategemezi kwa Mungu.
(viii) Maswali ya balagha ili kuwahusisha zaidi/kuteka hisia zao.
(ix) Lugha ya mafumbo/matumizi ya majazi.
(x) Kurudia vifungu/baadhi ya maneno kama vile ‘Amina’.
(xi) Anaweza kutumia misimu ya vijana iii kujinasibisha nao.
(xii) Matumizi ya ucheshi/ utani kiasi cha haja.
(xiii) Lugha ya unyenyekevu/ upole/ kusihi.
(xiv) Kutumia lugha sahili kulingana na kiwango cha wanafunzi.
(xv) Matumizi ya msamiati wa shuleni.