INSHA 102/1
1.Lazima :
Wewe ni mwenyekiti wa jopo lililoteuliwa kuchunguza chanzo cha utovu wa usalama kijijini Sokoto. Andika ripoti maalum /rasmi kuhusu jambo hili.
2.Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha. Jadili.
3.Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchagua nazi hupata koroma.
4. Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…
Mwongozo Wa Kusahihisha Insha Karatasi 102/1
1. Atambue kuwa ni swali la ripoti rasmi. Lazima insha hii iwe na anwani iliyo wazi, yaani iwe na neon ripoti, ya nani, kuhusu nini na wapi ?
Sharti sura ya ripoti maalum au rasmi izingatiwe:Kichwa, utangulizi, taratibu/yaliyoshughulikiwa, mwili/matokeo ya uchunguzi,hitimisho,mapendekezo na sahihi. Baadhi ya hoja:
Insha iwe na maudhui yasiyopungua matano. Baadhi ya hoja ni kama vile:UleviUkosefu wa kaziWanyama wa pori kama vile ndovuWatoto kutopelekwa shuleUtepetevu wa vyombo vyombo vya usalamaAdhabu nyepesi zinazotolewa na mahakamaWazazi kutotekeleza wajibu wao kwa watotoTamaduni zilizopitwa na wakati kama tohara, wizi wa mifugo n.k
Sharti mtahiniwa atoe mapendekezo ya kutatua tatitzo hili k.vKupiga marufuku utengenazaji na unywaji wa pombe haramuKuanza miradi ya kuajiri vijanaWatoto wote kupelekwa shuleVyombo vya usalama kuwa macho na kupigana na uhalifuAdhabu kali kutolewa kwa wahalifuWazazi kutekeleza wajibu wao wa kutunza watotoKukabiliana vikali na makundi haramuKutupilia mbali tamaduni zilizopitwa na wakati
Asiyezingatia sura ya ripoti aadhibiwe kwa kuondolewa 4s
Makosa ya sarufi na hijai yaadhibiwe yanapotokea
2.Mtahiniwa aandike insha ya hojaSharti ataje hoja, kuifafanua na kuitolea mifanoLazima aunge mkono hoja aliyopewaPia aonyeshe upande wa pili wa hoja aliyopewa.Aeleze mitindo ya maisha ya kisasa.Hoja zake ziwe tano au zaidi
Hoja za kuunga mkono:
i) Baadhi ya vyakula hasa vyenye mafuta, madini,sukari na chumvi husababisha magonjwa kama vile msukumo wa damu na kisukari
ii) Kukosa mazoezi ya mwili hasa kwa sababu ya matumizi ya magari ya usafiri na ya kibinafsi na watu hawatembei kwa miguu.
iii) Matumizi ya pombe huleta madhara mengi kwa mwili yanayosababisha magonjwa ya akili.
iv) Mienendo mibaya hasa kushiriki mapenzi ovyo ovyo husababisha magonjwa ya ukimwi, kisonono na magonjwa mengine ya zinaa.
v) Uchafuzi wa mazingira husababisha magonjwa kama vile ya pumu,malaria ,kipindupindu n.k Hoja za kupinga:
i) Atetee kwamba magonjwa hayasababishwi tu na mitindo ya maisha ya kisasa.
ii) Baadhi ya magonjwa hurithishwa katika familia.
iii) Kuna magonjwa yanayoletwa na wadudu kama vile mbu, konokono n.k
iv) Magonjwa kama vile mafua husababishwa na hali ya anga na si hali ya maisha.
v) Hali za kimaumbile kama vile mafuriko husababisha magonjwa kama vile kipindupindu.
3.Sharti aelewa kuwa ni methali.Atunge kisa ambacho kinaoana vizuri na maana ya matumizi ya methali hii.Kisa chake kiwe cha kuvutia.Sharti aonyeshe pande mbili za methali.Aonyeshe mhusika anayechagua kitu au jambo zuri lakini analikosa na kupata lingine la kiwango cha chini.Anatakiwa kuonyesha kuwa tusiwe watu wa kuchagua vitu bali tufanye bidii kupata tunachokihitaji.Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea
4. Ni sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa.Anatakiwa kuanza kwa maneno yale bila ya kubadilisha wala kuyapunguza. Kisa chake kiwa cha kuvutia na aonyeshe ni matukio yapi yaliyosababisha milipuko ile,kulikuwa na majeruhi na watu walitoroka kwenda wapi? Ni nini kilichotokea baada ya hapo?Asipoanza kwa maneno aliyopewa atuzwe alama ya bakshishi
BK01 USAHIHISHAJI KWA JUMLASharti mtahiniwa ajibu maswali mawili pekee.Kazi ya mtahiniwa iwe nadhifu na ipangwe vizuri kiaya.Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea.Baada ya kusahihisha kazi ya mtahiniwa, awekwe kwenye viwango ya A-D vilivyowekwa na baraza la kitaifa la mitihani K.N.E.CMtahini atakayepotoka, atakayejitungia swali au atakayetumia lugha isiyo Kiswahili atuzwe alama ya BK01.Urefu wa insha sharti uzingatiwe (maneno 400) 14Urefu ukadiriwe hivi:
Maneno | 100 | 200 | 300 | 400 |
---|---|---|---|---|
Kiwango | 14insha | 12insha | 34insha | Kamili |
Alama za juu | 05 | 10 | 15 | 20 |
Tanbihi:
i) Hizi ndizo alama za juu iwapo mtahiniwa ameandika kiwango hicho cha maneno . Kisha aadhibiwe makosa mengine
ii) Mtindo wa zamani wa kuondoa alama 2U ulitupiliwa mbali.
Alama zifuatazo zitumiwe katika usahihishaji.
✔ Msamiati unaofaa
× Msamiati usiofaa
– Kosa la hijai
═ Kosa la sarufi
^ Alama ya achwa – neno linapoachwa katika sentensi