2022 KCPE Past Papers- Kiswahili Past Paper with Marking Scheme

KCPE 2022 Past Papers- Kiswahili Past Paper with Marking Scheme

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

            Ijumaa     1      tulimtembelea Fauzia. Tulipofika kwake     2      kwa mikono miwili.    3     sebuleni ambapo tuliipata familia yake pamoja wakitazama kipindi fulani       4     runinga. Tuliandaliwa      5     wali, nyama, mboga na matunda.     6     mwenyeji kupiga dua, tulianza kula. Tulipomaliza chakula    7    tulishauriana na mwenyeji wetu na    8     kuhusu mradi wetu wa maji     9     utakinufaisha kijiji chetu. Kisha tukamuaga alamsiki naye akatujibu    10   .

1A. ilikopitaB. iliyopitaC. ilimopitaD. iliopita
2A. tunakaribishwaB tutakaribishwaC. tulikaribishwaD. tumekaribishwa
3A.TulielekezanaB. TulielekezewaC. TulielekezaD. Tulielekezwa 
4A. kwenyeB. penyeC. ndani yaD. kati ya
5 ,–  :
6A. JapoB. Licha yaC.Baada yaD. Sembuse
7A. yoteB. woteC. zoteD. chote
8A. kukata kauliB. kukata kiuC. kukata notisiD. kukata mate
9A. ambayeB. ambaoC. ambaloD. ambayo
10A. Sabalkheri!B. buriani!C. binuru!D. Masalkheri!


            Tunapaswa kuwa na moyo wakusaidiana    11    ilivyokuwa zamani.    12    mmoja wetu     13     msaada kwa ajili ya jambo fulani, inafaa tumsaidie bila   14    . Tukifanya hivyo, tutakuwa pia tunajiwekea akiba maishani kwani    15    .

11A. angaaB. ilimradiC. hataD. kama
12A. IngawaB. IkawaC. IwapoD. Ijapokuwa
13A. anahitajiwaB. anahitajiC. anahitajikaD. anahitajia
14A. kinyongoB. harakaC. huzuniD. kisasi
15A. wema huzaa wema.B.akili ni mali.C. mkono mtupu haulambwi.D. subira huvita heri.


Kutoka nambari 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

  1. Neno, ‘tulimpokea’ lina silabi ngapi
    1. 4
    2. 5
    3. 10
  2. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:
    Mti ule wa mchungwa ulizaa tunda tamu.
    1. Mti ule wa mchungwa ulizaa matunda matamu.
    2. Miti ile ya michungwa ilizaa tunda tamu. 
    3. Miti ile ya michungwa ilizaa matunda matamu.
    4. Mti ule wa mchungwa ulizaa matunda tamu.
  3. Chagua jibu sahihi:
    ‘Wachezaji wa soka huhimizana kufanya mazoezi kila siku’. ‘na’ imetumika kuonyesha:
    1. Kufupishwa kwa viwakilishi nafsi. 
    2. Hali ya kukubaliana katika jambo.
    3. Wakati usiodhihirika kwenye kitendo.
    4. Mnyambuliko wa kauli ya kutendana.
  4. Ni sentensi ipi ambayo inaunganisha sentensi zifuatazo ipasavyo.
    Tamira alipika wali. Wali ulikuwa kwa Riziki.
    1. Wali ulipikwa kwa Riziki na Tamira.
    2. Tamira alipikiwa wali kwa Riziki.
    3. Riziki alipikiwa wali kwa Tamara
    4. Wali ulipikwa kwa Tamira na Riziki.
  5. Ni jibu lipi lenye methali zenye maana sawa?
    1. Chanda chema huvikwa pete.
    2. Chumia juani ulie kivulini. 
    3. Mcheza kwao hutuzwa.
    4. Mfuata nyuki hakosi asali.
      1. (i) (iv)
      2. (ii) (iv)
      3. (i) (iii)
      4. (ii) (iii)
  6. Chagua jibu lisilo ambatanishwa ipasavyo.
    1. – zito kama ndovu
    2. mbio kama duma
    3. – eusi kama mpingo
    4. chungu kama shubiri
  7. Ni kundi lipi la nomino ambalo lipo katika ngeli ya YA-YA
    1. maisha, maagizo
    2. marashi, maarifa
    3. maji, maembe
    4. maskani, mavazi
  8. Rudi ni kurejea ulipokuwa umetoka. Rudi pia ni:
    1. jambo kufanyika mara nyingine.
    2. nguo kuwa fupi baada ya kufuliwa. 
    3. msamaha unaotolewa baada kukubali makosa. 
    4. kitendo cha kubingiria kutoka mlimani.
  9. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri:
    1. Hoyee, Mtoto amecheka kweli? 
    2. Je? Unamfahamu karani huyu.
    3. Farida alinunua vifaa vifuatavyo: kitabu, kalamu na kifutio.
    4. Wachezaji walishangilia! baada ya ushindi huo jana jioni.
  10. Jesca anaishi kilomita moja kaskazini mashariki mwa shule yetu. Kibibi naye anaishi kilomita moja kusini mwa shule hiyo. Je, Kibibi anaishi upande gani wa Jesca?
    1. Kaskazini mashariki
    2. Kaskazini magharibi
    3. Kusini mashariki
    4. Kusini magharibi
  11. Kauli, ‘Lugogo ni samaki majini’, imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. nahau
    2. sitiari
    3. tashihisi
    4. kinaya
  12. Chagua jibu lenye nomino ya makundi isiyofaa.
    1. Mzengwe wa nyuki.
    2. Thurea ya nyota.
    3. Kishazi cha samaki.
    4. Shungi la nywele.
  13. Onyesha sentensi yenye kivumishi.
    1. Mwajuma alisafisha darasa jana. 
    2. Gari limefika mapema.
    3. Kule kuna miti mirefu.
    4. Wawili walisajiliwa chuoni.
  14. Ni jibu lipi lenye mapambo ya puani pekee?
    1. Jebu, kipuli
    2. Usinga, udodi
    3. Furungu, njuga
    4. Kipini, kikero
  15. 5/6 kwa maneno ni
    1. sudusi sita
    2. humusi sita
    3. sudusi tano
    4. humusi tano

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

            Mawasiliano ni njia ya kupashana habari kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Sijui kama umewahi kuwazia namna watu wa kale walivyotekeleza mchakato huu wa mawasiliano. Kwangu ninaona njia za mawasiliano zilikuwa za ajabu mno. Hebu fikiria kufuka kwa moshi kama ishara ya ujumbe fulani. Je, unafahamu pia milio mbalimbali ilipitisha habari muhimu katika jamii hizo? Kumbuka mbiu ya mgambo wanasema ikilia kuna jambo. Hakika suala la mawasiliano ni nguzo muhimu katika maisha ya binadamu.
            Ulimwengu wa sasa umepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Maendeleo hayo yameleta mabadiliko makuu katika mawasiliano. Mfumo wa mawasiliano umewaunganisha waja katika shughuli zao za kila siku. Ilikufanikisha a mawasiliano baina yao, jambo la kimsingi huwa ni kupitisha ujumbe. Wewe mwanafunzi, unapokuwa shuleni kunazo habari muhimu unazohitajika kumfikishia mzazi au mlezi wako. Je, unazifikisha vipi habari hizo?
            Fikiria kuhusu wale wanaofanya kazi mbali na familia zao. Unadhani wanawafikishia wapendwa wao taarifa kwa njia gani? Kuna njia nyingi za kuwasilisha ujumbe. Kwa mfano kupiga simu. Vyombo vya habari navyo vinatuwezesha kupitisha ujumbe. Kila siku vinatupasha habari za kila aina. Ni vyema tufahamu kuwa ili mawasiliano yakamilike, basi ujumbe sharti umfikie mlengwa. Mlengwa naye anafaa kuufahamu ujumbe uliokusudiwa.
            Tunapopokea ujumbe, tutafakari kuhusu yule aliyetuma ujumbe na ujumbe wenyewe. Sababu kuu ni kubaini lengo kuu la mawasiliano yake. Je, amekusudia nini? Wengi wanaopokea ujumbe wanashindwa kumwelewa aliyetuma ujumbe kutokana na hali ya ujumbe wake. Lugha aliyoitumia inaweza kuwa na utata ambao unatinga kueleweka kwa ujumbe huo. Wengine wanatumia lugha ya mafumbo ambayo labda haieleweki na mlengwa wa ujumbe. Wazia kuwa umemwomba rafiki yako akununulie mbuzi kwa kuwa unahitaji kumfuga nyumbani, kisha ujumbe huu umpige chenga akuletee
kifaa cha kukunia nazi.
            Je, utamlaumu au utamcheka mpaka mbavu zivunjike? Iwapo tunahitaji kufanikisha mawasiliano, basi ni muhimu tutumie lugha inayoeleweka vyema. Tukumbuke kuwa, katika lugha, maneno huwa na maana mbalimbali katika muktadha.
            Hali ya mpokezi wa ujumbe inaweza kuwa kikwazo cha mawasiliano. Huenda anayepokea ujumbe amekumbwa na hali ambazo zinamkosesha utulivu wa kimawazo. Hali hizo zinaweza kuwa matatizo ya kiafya, majukumu ya malezi na kazi miongoni mwa mengine. Hali hii inaweza kutatiza mkondo wake wa mawazo akakosa makini ya kuufahamu ujumbe uliokusudiwa. Mazingira aliyomo mpokezi wa ujumbe huo, huenda pia yakaathiri uelewa wa ujumbe. Chukulia kwa mfano, umetumwa gulioni kununua bidhaa. Kama ilivyo kawaida, maeneo kama hayo huwa na halaiki ya watu na kelele nyingi. Si muziki, si matangazo ya kibiashara, si mahubiri, yataje yote. Ukipigiwa simu wakati kama huo unaweza kukosa kuisikia. Iwapo utaisikia upokee, mawasiliano yatatizika bila shaka.
            Kufanikiwa kwa shughuli nzima ya mawasiliano kunategemea iwapo aliyetuma ujumbe amepokea majibu kwa mujibu wa ujumbe wake. Ni vyema basi tutafakari kuhusu vikwazo vyote ambavyo vinatatiza mawasiliano. Tukumbuke kuwa mawasiliano yetu hutegemea mahusiano yetu, viwango vyetu vya elimu, mila na desturi na chombo cha mawasiliano kinachotumika miongoni mwa mengine. Kila kipengele kitiliwe maanani kwa kuwa ufanisi wa mawasiliano utategemea uelewa wa ujumbe.

  1. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya kwanza:
    1. Mwandishi anawahurumia watu wa enzí ya zamani.
    2. Maisha bora ya jamii hutegemea namna tunavyowasiliana na watu wengine.
    3. Utaratibu wa sasa wa kupitisha habari ni bora kuliko wa zamani.
    4. Upashanaji wa habari wa kale uliwashangaza wengi.
  2. Kulingana na aya ya pili:
    1.  Mahitaji mbalimbali ya wanajamii yamezua mbinu nyingi za kupashana habari.
    2. Taarifa kutoka shuleni zinachangia uelewa wa mambo ya nyumbani.
    3. Upashanaji wa habari katika jamii hutegemea wanahabari wenyewe.
    4. Ustawi wa jamii unategemea vifaa vya Akiteknolojia pekee.
  3. Kulingana na kifungu:
    1. Wahenga waliulizana maswali mengi kuhusu upashanaji wa habari.
    2. Matarajio ya mpokezi wa ujumbe My huathiri ufahamu wa taarifa.
    3. Upataji wa habari kwa wepesi hutegemea ufahamu wa ujumbe.
    4. Lugha tofauti anazozijua mpokezi way ujumbe humwezesha kupokea habari.
  4. Ni kauli ipi si sahihi kulingana na aya ya tatu?
    1.  Msingi wa upashanaji habari ni kufahamu madhumuni ya anayetuma taarifa.
    2. Kutumia lugha fiche katika ujumbe huharibu uhusiano wa kijamii.
    3.  Kiwango cha lugha katika ujumbe huweza kutatiza uelewa wa habari.
    4. Kutoelewa ujumbe kuna madhara kwa anayetuma na kupokea habari.
  5. Kifungu kimebainisha kwamba:
    Mawasiliano
    1. yanafaidi wenye simu.
    2.  yanaleta familia pamoja.
    3. hufaulu mahali penye utulivu.
    4. humfanya mtu afikirie sana.
  6. Aya ya nne imebainisha kwamba:
    1. Utaratibu wa kupashana habari hutegemea namna mtu anavyofikiria kuhusu maisha.
    2.  Kazi anazofanya mtu hutatiza jinsi anavyopokea ujumbe.
    3. Mahali alipo anayetuma ujumbe huweza kuathiri uelewa wa taarifa lengwa.
    4. Upokeaji ujumbe kwa usahihi hutegemea umakinifu wa mpokezi.
  7. Kwa mujibu wa kifungu, lugha ya mawasiliano inafaa
    1.  iwe wazi na rahisi kwa mpokezi. 
    2. iwe ya kumvutia mpokezi na yenye mafumbo.
    3.  kuleta maana mbalimbali kwa mpokezi.
    4. kutuliza fikira za mpokezi wa ujumbe.
  8. Maoni ya mwandishi katika aya ya mwisho ni kwamba:
    1. Ukamilifu wa mawasiliano huamuliwa na muda anaochukua mpokezi kutoa jawabu.
    2.  Mawasiliano baina ya binadamu katika jamii huathiriwa na utamaduni wao.
    3. Ujumbe unaopitishwa kwa vifaa vya mawasiliano pekee ni bora zaidi.
    4. Vizuizi vya mawasiliano hutokea pale tunapowaza kuhusu hali ya mpokezi.
  9. Kauli ‘umpige chenga’ imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. sitiari
    2. tashbihi
    3.  nahau
    4. tashihisi
  10. Maana ya, ‘halaiki ya watu’  kulingana na kifungu ni:
    1. Watu wenye mienendo inayofanana.
    2. Watu wengi waliokusanyika pamoja.
    3. Wataalamu wenye maarifa mengi.
    4. Wauzaji wa bidhaa sokoni.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.


Sound
             Mimi na Mwamba tulijiunga na shule ya msingi ya Maarifa wakati mmoja. Tangu wakati huo nimemtambua Mwamba kama rafiki wa kuaminika. Tulisoma pamoja, tukacheza pamoja na kushirikiana katika mambo mengi. Alikuwa mmakinifu, msikivu na mchangamfu. Unadhifu wake uliwavutia wengi. Hata mimi aliniathiri nikamuiga. Walimu na wanafunzi walimshabikia na kumthamini hata wakamchagua kuwa kiongozi. Vipawa vya Mwamba vilianza kuchipuka mapema.Naye Mwamba alijitahidi kuvipalilia.
             Bidii ya Mwamba inaweza kumithilishwa na ile ya mchwa kujenga kichuguu kwa mate. Mwamba alifahamu fika kuwa mja yeyote kujaliwa ni yeye mwenyewe kujipa uvumilivu, kutia bidii na kushirikiana na wenzake. Alifanya juu chini kuelewa yote tuliyofundishwa na walimu wetu. Ingawa akili yake ilikuwa kama sumaku, pale ambapo alitatizika kuelewa hakufa moyo. Alikuwa tayari wakati wote kujadiliana na wenzake katika vikundi. Alitambua kuwa jifya moja haliinjiki chungu. Pamoja na hayo, Mwamba alijaliwa moyo wa kusaidia. Wakati mwingine katika kundi letu alitufafanulia mada ambazo hatukuzielewa vizuri. Aliwafaa hata wale waliokuwa na changamoto ya kuelewa yaliyofunzwa na walimu. Ama kwa hakika, tulishangazwa na subira na unyenyekevu wake.
             Mimi na rafiki yangu Mwamba tulijiunga na timu ya soka ya shule yetu. Alichukua nafasi ya mshambulizi nami nikawa mlinda lango. Kila tuliposhiriki kwenye mashindano, Mwamba aliifungia timu yetu mabao mengi. Mara nyingi, tuliibuka washindi na kuwaacha wapinzani wetu vinywa wazi. Nyota ya Mwamba ilianza kung’aa michezoni. Alipokea tuzo ya mwanasoka bora zaidi katika gatuzi letu. Nayo timu yetu ilinyakua kombe la ushindi na sare kamili za kandanda. Shule yetu ilisifika na kutambulika kama kitovu cha wachezaji kandanda chipukizi. Hata baadhi yetu tulichaguliwa kujiunga na timu ya kitaifa ya vijana.
             Mwaka huu, Mwamba amegundua kipawa chake kingine katika rubaa ya muziki baada ya kujiunga na bendi ya muziki shuleni. Wakati wa gwaride na pia sherehe mbalimbali shuleni ameweza kupata nafasi ya kututumbuiza. Sauti yake ya kinanda na nyimbo zake zimevuma kotekote. Kuvuma kwa nyimbo hizo kunatokana na ujumbe wa nyimbo zake. Nyimbo hizo huwahimiza watu kukuza maadili na bidii kila uchao. Hakika, zinatuliza mioyo, zinahimiza, zinachochea watu kuwa na upendo, amani na ushirikiano. Katika siku za hivi majuzi bendi yao imetunga nyimbo ambazo zimevutia wafuasi wengi mitandaoni. Baadhi ya vituo vya mawasiliano vimetuma maombi kualika bendi hiyo kwenye studio zao. Azma yao ni kurekodi baadhi ya nyimbo zao ili zitumike kama milio kwenye simu zinapopigwa au kukiriza. Aidha nyimbo zao huchezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga. Chini ya uongozi wa mwalimu wao, ambaye ni mlezi wa bendi yao, wameweza kujipatia hela ambazo zimetumika kununulia vyombo zaidi vya muziki. Mwalimu huyu wao huhakikisha kuwa bendi hiyo ina nidhamu ya hali ya juu.
             Juma lililopita, mwalimu wa zamu aliwapa nafasi wanafunzi kadha kutoa nasaha kuhusu namna ya kufanikiwa masomoni. Mwamba alikuwa miongoni mwao. Hotuba yake ililenga ndipo. Alisema, “Wanafunzi wenzangu, kufaulu kwetu masomoni na pia maishani hakutegemei kule tulikotoka bali nidhamu ya mtu mwenyewe”. Alituambia kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa. Kwa hivyo, tujitahidi masomoni. Aliongezea kusema kuwa, kila mtu amejaliwa muda wa saa ishirini na nne kila siku. Alituhimiza tuuratibu muda wetu vyema. Katika kuhitimisha hotuba yake alisisitiza tuwaheshimu wakubwa wetu ili tuweze kufanikiwa maishani. Hotuba yake hupigiwa debe shuleni hadi leo.

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza:
    1. Sifa nzuri za mtu humfanya kutambulikana na wengi.
    2.  Wanafunzi wote shuleni walifuata mienendo ya Mwamba.
    3. Viwango vya usafi shuleni viliimarishwa na Mwamba.
    4. Vipaji vya Mwamba vilikuzwa na wenzake wakiwa shuleni.
  2. Aya ya pili imebainisha kwamba:
    1.  Mpango wa Mwamba wa kutoa mafunzo ya ziada uliwavutia wote shuleni.
    2. Kufanya jambo kwa pamoja shuleni kulileta mafanikio kwa Mwamba na wenzake.
    3. Mwamba alikuwa na uwezo wa kufahamu yote yaliyofunzwa shuleni kwa wepesi.
    4.  Kustaajabia ujuzi wa Mwamba kuliwafanya wanafunzi wote wam- heshimu zaidi.
  3. Chagua jibu lisilo sahihi’ kwa mujibu wa aya ya tatu:
    Ushindi wa timu ya soka ya shule ya Maarifa
    1. uliwapa wachezaji nafasi ya kukuza vipawa vyao.
    2. uliwawezesha wachezaji kutambuliwa katika kiwango cha gatuzi lao.
    3. ulifanya shule ya Maarifa kujulikana na wengi.
    4. ulitegemea ustadi wa soka aliokuwa nao Mwamba pekee.
  4. Kifungu kimebainisha kwamba:
    1. Matumaini ya mtu maishani huchangia kufanikiwa kwake.
    2. Uongozi hutegemea idadi ya talanta alizonazo mtu.
    3. Kutambua talanta moja mapema kunamwezesha mtu kuwasaidia wengine kuzua vipaji vyao.
    4. Kuvuma kwa shule ya Maarifa kulito- kana na nyimbo za bendi yake.
  5. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya nne:
    1.  Kila mwaka, Mwamba na wenzake walishirikiana kutambua vipaji vyao.
    2. Vyombo vya habari viliongezea mapato yake kutokana na nyimbo za Mwamba.
    3. Walimu wana jukumu la kuweka msingi mzuri kukuza vipaji vya vijana.
    4. Kualikwa kwa wanabendi studioni kulitegemea vifaa vingi vya muziki walivyonunua.
  6. Mwamba ni mfano bora kwa wenzake kwa kuwa:
    1. Walifuata matendo yake mema.
    2. Walijiunga na bendi ya shule.
    3.  Alialikwa kwenye vituo vya habari.
    4. Alihifadhi fedha alizopata kutokana na muziki.
  7. Lipi si jibu sahihi kulingana na aya ya mwisho.
    Kufaulu masomoni kunategemea:
    1. Matumizi ya muda wetu.
    2. Mazingira ambayo tumelelewa.
    3. Maamuzi tunayofanya kuhusu elimu yetu.
    4. Mawaidha tunayopata kutoka kwa wenzetu.
  8. Chagua mfuatano sahihi wa matukio yafuatayo kulingana na kifungu.
    1. Mwamba kupokea tuzo.
    2. Mwamba kujiunga na bendi ya muziki. 
    3. Nyimbo za Mwamba kuvuma.
    4. Mwamba kujiunga na timu ya soka.
    5. Nyimbo za Mwamba kuchezwa kwenye vituo vya habari.
      1. (ii) (iii) (v) (iv) (i)
      2. (iv) (iii) (v) (ii) (i)
      3. (ii) (iv) (i) (iii) (v)
      4. (iv) (i) (ii) (iii) (v)
  9. . Kauli, ‘akili yake ilikuwa kama sumaku’ imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. sitiari
    2.  tashbihi
    3. nahau
    4. chuku
  10. Hotuba ya Mwamba hupigiwa debe shuleni mwetu hadi leo ina maana kuwa:
    1. Inasisitizwa kila wakati.
    2. Inashangiliwa mara nyingi.
    3. Inafurahiwa na wote shuleni. 
    4. Inafundishwa katika kila darasa.

Majibu


1.B11.D21.A31.B41.A
2.C12.C22.B32.A42.B
3.D13.B23.B33.C43.D
4.A14.A24.C34.B44.C
5.D15.A25.D35.C45.C
6.C16.C26.B36.D46.A
7.D17.C27.A37.A47.B
8.A18.D28.C38.B48.D
9.B19.A29.D39.C49.B
10.C20.C30.C40.B50.A