Maswali
MAAGIZO
• Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
• Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
• Kila insha isipungue maneno 400.
• Kila insha ina alama 20.
• Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
- Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
- Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo.
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.
Mwongozo wa kusahihisha
- TAWASIFU
Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
SURA
• Atumie nafsi ya kwanza
• Atumie aya kuwasilisha hoja zake
• Maisha ya kuzaliwa, kukua na elimu ichukue nafasi ndogo katika tawasifu
• Mtahiniwa ashughulikie ufaafu wake.
BAADHI YA MAUDHUI
• Yeye mwenyewe kwa mtoto wa kurandaranda
• Aokolewa na ajiunga na elimu
• Kuwa kiongozi wa shirika la kusaidia watoto shleni — aelezee shughuli walizohusika nazo
• Shahada yake ni kuhusu nini?
• Baada ya kuhitimu ameshughulikia mradi ipi?
• Je kuna masuala aliyochangia kimaadhishi
• je amehusika na makao mangapi ya watoto wanaorandaranda
Tashbihi
• Akitumia mtindo wa hotuba kama vile salamu hana sura — 4mm ( sura)
• Lazima atumie nafsi ya kwanza
• Akikosa — 4 mm (sura)
- Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha SURA
• Hili ni swali elekezi kila hoja itajwe, ifafanuliwe na ikamilike
• Ikiwa hoja haija kamilika isituzwe
• Lazima mtahiniwa awe na hoja zaidi ya saba kuhitimisha maudhui
• Lazima atumie hoja mufti
BAADHI YA HOJA
• Hufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu
• Hufanikisha biashara
• Hufanikisha elimu
• Hukuza utangamano
• Kuboresha mahusiano
• Kuboresha usalama
• Huburudisha — husaidia watu kukabiliana na matatizo k.v msongo wa mawazo n.k
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
• kisa kinafaa kioana na methali
• Mwanafunzi azingatie methali husika
• maana ya hiyo iwe anayekutangulia si lazima akamilishe mkondo anaweza kukosa kufika
• mtahiniwa atunge kisa kimoja
• aonyeshe sehemu zote mbili za methali
• dhana ya kutangulia ionekane vizuri
• dhana ya kutofika ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja
- Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele. jibu
• Mtahiniwa ajikite katika kisa ambacho kinaelezea mambo magumu ambayo yamezunguka maishani hadi kufikia upeo wa ufanisi
• Mtahiniwa pia aeleze namna ambavyo amefanikiwa maishani baada ya masaibu mengi
• Kisah kisimuliwe katika nafsi ya kwanza