2022 Mock Examinations Kiswahili Paper 1 with Answers-Kapsabet High School

Maswali

MAAGIZO

• Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.

• Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.

• Kila insha isipungue maneno 400.

• Kila insha ina alama 20.

• Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

  1. Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
  2. Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
  3. Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
  4. Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo.

Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.

Mwongozo wa kusahihisha

  1. TAWASIFU

Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.

SURA

• Atumie nafsi ya kwanza

• Atumie aya kuwasilisha hoja zake

• Maisha ya kuzaliwa, kukua na elimu ichukue nafasi ndogo katika tawasifu

• Mtahiniwa ashughulikie ufaafu wake.

BAADHI YA MAUDHUI

• Yeye mwenyewe kwa mtoto wa kurandaranda

• Aokolewa na ajiunga na elimu

• Kuwa kiongozi wa shirika la kusaidia watoto shleni — aelezee shughuli walizohusika nazo

• Shahada yake ni kuhusu nini?

• Baada ya kuhitimu ameshughulikia mradi ipi?

• Je kuna masuala aliyochangia kimaadhishi

• je amehusika na makao mangapi ya watoto wanaorandaranda

Tashbihi

• Akitumia mtindo wa hotuba kama vile salamu hana sura — 4mm ( sura)

• Lazima atumie nafsi ya kwanza

• Akikosa — 4 mm (sura)

  1. Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha SURA

• Hili ni swali elekezi kila hoja itajwe, ifafanuliwe na ikamilike

• Ikiwa hoja haija kamilika isituzwe

• Lazima mtahiniwa awe na hoja zaidi ya saba kuhitimisha maudhui

• Lazima atumie hoja mufti

BAADHI YA HOJA

• Hufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu

• Hufanikisha biashara

• Hufanikisha elimu

• Hukuza utangamano

• Kuboresha mahusiano

• Kuboresha usalama

• Huburudisha — husaidia watu kukabiliana na matatizo k.v msongo wa mawazo n.k

  1. Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”

• kisa kinafaa kioana na methali

• Mwanafunzi azingatie methali husika

• maana ya hiyo iwe anayekutangulia si lazima akamilishe mkondo anaweza kukosa kufika

• mtahiniwa atunge kisa kimoja

• aonyeshe sehemu zote mbili za methali

• dhana ya kutangulia ionekane vizuri

• dhana ya kutofika ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja

  1. Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo

Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele. jibu

• Mtahiniwa ajikite katika kisa ambacho kinaelezea mambo magumu ambayo yamezunguka maishani hadi kufikia upeo wa ufanisi

• Mtahiniwa pia aeleze namna ambavyo amefanikiwa maishani baada ya masaibu mengi

• Kisah kisimuliwe katika nafsi ya kwanza