KCPE 2020 Kiswahili Past Paper-Free KCPE Past Papers with Answers

Kenya Certificate of Primary Education

Kiswahili

Sehemu ya Kwanza

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Mtu __1__ lugha huanza kwa kutamka sauti za lugha hiyo. Sauti hizo huambatana __2 kuunda silabi. Neno __3 _ kwa idadi maalum ya silabi. Mathalani, neno, ‘iliyowambwa’ lina silabi__4 _Mtumiaji wa lugha pia hujifunza viambishi vya aina mbalimbali. Kwa mfano, ‘ku’ katika, ‘alikutarajia ufike’ inaonyesha___5 _ Maneno __6 _ ni muhimu katika kuwasiliana. Kwa mfano, neno ‘hewala’ ambalo ni__7__ huonyesha __8

1. A. analojifunza B. anayojifunza C. anaojifunza D.✔anapojifunza

2. A.✔ ili B. maaadam C. lau D.minajili

3. A. hujengwa B. hujenga C.✔ hujengwa D.hujengea

4. A. 4 B.✔ 5 C. 6 D. 3

5. A. kitenzi B. wakati C. mahali D.✔ nafsi

6. A. nao B. nazo C.✔ nayo D. nako

7. A. kielezi B.✔ kihisishi C. kiunganishi D. kivumishi

8. A.✔ kukubaliana na jambo C. kuomba kitu kisimuumize mtu

Lugha __9 _ mazingira anamoishi binadamu. Huwa na misamiati mbalimbali. __10 misamiati hii ni ya uhunzi kama vile kusana. Isitoshe, mwanafunzi hujifunza kuunda neno kutokana na__11__. Kutokana na nomino ‘mtu’ tunapata nomino ‘utu’ ilhali kivumishi ‘nyepesi’ huunda nomino __12 _. Mwanafunzi huandika sentensi katika kauli tofautitofauti. Sentensi, ‘Afisa alikagua cheti cha Hamu’ katika kauli ya kutendea ni __13__. Ushairi pia ni kipengele cha lugha__14 _ huwachangamsha wanafunzi. Mashairi kama vile __15__ huwa na mishororo mitano katika kila ubeti.

9. A. huelezeka B. huelezwa C. huelezewa D.✔ lnelezea

10. A. Mbali na B.✔ Baadhi ya C. Mkabala na D. Zaidi ya

11. A. nyingine B.✔ lingine C. mwingine D. kwingine

12. A. jepesi B. upesi C.✔ wepesi D. mwepesi

13. A. Afisa alikagulia cheti kwa Hamu B.Cheti kilikaguliwa Hamu kwa Afisa ambacho

C. Cheti kilikaguliwa Hamu na Afisa D.✔ Afisa alimkagulia Hamu cheti

14. A.✔ ambacho B. ambao C. ambayo D.ambalo

15. A. tathnia B. tathlitha C.✔ takhmisa D. tasdisa Kutoka swali 16 mpaka 30 chagua jibu sahihi.

16. Chagua wingi wa: Chifu atamwongoza kushughulikia jambo hilo kijijini.

A. Chifu atawaongoza kushughulikia jambo hilo vijijini.

B. Chifu atawaongoza kushughulikia mambo hayo vijijini.

C. ✔ Machifu watawaongoza kushughulikia Mainbo hayo vijijini.

D. MaChifu watawaongoza kushughulikia jambo hilo vijijini.

17. Ni sentensi ipi iliyotumia ‘na’ kama kiunganishi?

A. Uchumi utaimarishwa na wananchi wote.

B. Ukumbi huo una waigizaji wengi.

C. Hao wanaandikiwa barua kutoka ughaibuni.

D. ✔ Amosi aliwapikia na kuwapakulia chakula hicho.

18. Chagua kitenzi chenye kiwakilishi ‘wa’ cha mtenda.

A. ✔ watamchezea

B. aliwakaribisha

C. tuliwahimiza

D. uliwasoıneshea

19. Ni sentensi ipi iliyotuınia wakati uliopita hali timilifu?

A. Ngao hii itakuwa imetumika kabla ya mashindano ya mwakani.

B.✔ Ngoma ile ilikuwa imepasuliwa baada ya wachezaji kupumzika.

C. Nguo yake ilikuwa inanunuliwa kabla ya sherehe hiyo.

D. Nyumba yao itakuwa inajengwa baada ya kuboniolewa.

20. Chagua ukanushaji wa sentensi ifuatayo: Mwale ananunua kanga akizipanga kwenye sanduku.

A. Mwale hajanunua kanga akizipangi kwenye sanduku.

B. Mwalc hakununua kanga akizipanga kwenye sanduku.

C. Mwale hatanunua kanga akizipanga kwenye sanduku.

D. ✔ Mwale hanunui kanga akizipanga kwenye sanduku.

21. Onyesha jibu lenye maneno ambayo si visawe.

A.✔ giza — mwangaza

B. vizuri — vyema

C. kidole — chanda

D. fika — wasili

22. Ni sentensi ipi yenye kivumishi cha pekee?

A. Mti huu ni mrefu ukilinganishwa na ule.

B. Kijana mtiifu atatuzwa na mlezi wake.

C.✔ Jembe lenyewe limevunjika mpini.

D. Nchi inahitaji askari wengi kudumisha usalaina.

23. Chagua jibu lisilotumia lnaneno ya adabu.

A. Mweke alihitaji kujisaidia kabla ya kuanza safari.

B. Juma atakuwa amekula chumvi nyingi katika umri huo.

C. ✔ Mtoto akihara na kukojoa damu huwa hatarini.

D. Kinyesi cha ndovu huwaelekeza watalii kwa kupitia.

24. Mjomba ni kwa shangazi ilhali buda ni kwa:

A. kigoli

B.✔ ajuza

C. ghulamu

D. shaibu Onyesha jibu lisiloambatanishwa ipasavyo.

25. Onyesha jibu lisiloambatanishwa ipasavyo.

A.✔ Ridhaa — malipo ambayo ıntu hupewa kwa kuokota kitu

B. Fidia — malipo anayopewa mtu aliyefikwa na hasara

C. Kiingilio — malipo anayotoa mhı kutazama mchezo uwanjani

D. Fainî — malipo anayotozwa mtu aliyepatikarıa na hatia.

26.Akisami 5/6 kwa maneno ni:

A. subui tano

B. tusui tano

C. thumni tano

D.✔ sudusi tano Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.

27. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.

A. Kaari ni bintiye shem: Kaari pia ni mwaliınu

B. “Kesi hii” akasenıa jaji itaamuliwa kesho.”

C. Nyimbo — nyingi zile za zamani — zinawavutia wengi.

D. ✔ Mashi (yule kijana aliyefuzu juzi) amekiletea kijiji hiki fahari. Kîdani ni kwa

28. Kidani ni kwa shingo ihlali _________ni kwa mkono.

A.✔ kikuku

B. hazama

C. kikuba

D. njuga

29.Konga ni ktizeeka, konga pia ni

A. kutumia mrija kuvuta kinywaji baridi.

B.✔ kuleta watu pamoja kwa shughuli fulani.

C. kupunguza hamu ya kitu usicho nacho.

D. kukubaliana na jambo ainbalo wengine wainelijadili.

30. Kauli iliyopigiwa mstari imetumia taıuathali gani ya uscmi?

Matone makali ya mvua yaliusalimia uso wake.

A. nahau

B. sitiari

C. ishara

D.✔ tashhisi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40 Bila shaka umewahi kushiriki katika michezo mbalimbali shuleni au kijijini. Hata hivyo, nikikuuliza kuhusu umuhimu wa michezo hiyo katika maisha yako huenda ukachukia sekunde moja au mbili kujibu. Kwa nini hali iwe hivyo?

Ni kwa sababu upo wakati katika maislıa yetu ya utoto na hata ya utu uzima ambao tunashiriki shughuli fulani kabla ya kuipa fikira ifaayo. Wakati mwingine tunajipata tukiuma vidole: tumejiponza kwa uamuzi wetu.

Sijui unajihisi vipi wakati aınbapo unaslıiriki na wenzako katika michezo kama vile kibe au ınwajificho.

Je, wakati aınbapo unajificlıa nyuma ya mlango wa sebule, mnuna au nılungizi wako akutafute kwa udi na uvumba asilcupate, unahisi vipi? Si, unajihisi kuwa shujaa au bingwa? Je, hili linakupa hamu zaidi ya kutafuta mikakati bora ya kujificha ili nao watafute mbinu bora zaidi za kukutafuta? Je, wakati unawasikiliza kutoka mafichoni wakikuita, “Mweledi, tafadhali jitokeze,” si unaingiwa na fahari kwa kuwa mshindi?” Hivyo ndivyo tıılivyohisi tulipoclıeza kibe zamani.

YunAini umewahi kuruslıa tiara kwenye uwanja wa shule. Huu ni mchezo ambao tuliupenda sana tukiwa watoto. Naktıınbuka wakati huo ningesimama katikati ya uwanja mkubwa wa michezo kijijini mwetu.

Ningeishika tiara yangu na kuitupa juu, naiamrislıa ipae. Tiara ingepaa kwa ınbwembwe juu huko mbinguni, inafika kileleni mwa mbingu jinsi kipungu afanyavyo.

Katika hali hii, licha ya kuburudika, ningejilıisi kana kwamba nauıniliki ulimwengu mzima; ııimeweza kuyadlıibiti ınaislıa yangu na kukidlıibiti chombo chenyewe. Najua pia umewahi kushiriki katika michezo nyingine ya watoto mama nilivyofanya.

I£uınbuka ulivyojifanya wewe ni mama, unawapikia na kuwafumia fulana watoto wako! Kuınbuka ulivyoona fahari wenzako walipokuita mama, nawe mnawahimiza kuwa na nidlıamu; wakati mwingine hata ımarnwigiza lnzazi wako kwa lcuwapiga! Najua nikikuuliza utaniambia kwamba michezo kama hii ilikusaidia kupalilia kipawa chako cha uigizaji. Haitakuwa ajabu ukiniambia kuwa hivi sasa wewe ni mwigizaji malıiri katika shule yako.

Ikiwa ulikulia katika kijiji ambamo familia zilijenga karibu karibu, utakumbuka jinsi aghalabu ınlivyokusanyika kila mchana na hata jioni kupitisha ınuda. Sijui kama uliwalıi kushiriki katika vikao vya kushindana utaınkaji wa vitanza ndimi, lnıtega na kutegua vitendawili, na hata kutambiana hadithi.

Ni dhahiri kwamba, licha ya vilcao hivi kuwaleta pamoja kanka wanakijiji, viliwaclıangamsha na kunoa bongo zenu. Najua utaniaınbia kuwa vikao hivi viliibııa uclıeslıi mkubwa. Kumbuka namına ulivyomcheka mwenzako wakati alipotaınka vibaya, naye akakukunıbusha jinsi ulivyoshindwa kuruka kaınba katika mchezo wa kuruka kamba! Ni wazi kwamba michezo ina ınanufaa nıakubwa kwako.

Ukipigia darubini maisha yako ya utotoni, utakumbuka ule mchezo wa kuketi katika duara huku mmoja wenu akikiınbia kuzunguka duara hiyo na kuınpokeza mmoja wenu zanıu yake kukimbia kwa kumpiga kwa kitambaa fulani begani au hata kichwani.

Mbio hizi si tofauti na zile wanazoslıiriki wakimbiaji hodari nchini. Pamoja na kunyooslıa misuli na kupumzislıa akili, mbio hizi huimarislıa afya ya anayeshiriki. Yeye kila mara hujihisi mwepesi kama unyoya.

Chakula anachokula hutumia vyema mwilini, hivyo kukinga dhidi ya kujinenepea ovyo. Usidhani ni mbio tu ambazo ni muhimu. Ipo michezo mingine kama vile uogeleaji na kandanda.

Nakumbııka kijijini tuliogelea na kupiga kachonıbe kwenye vidimbwi na ınabwawa ya kiasili. Siki hizi mınejengewa mabwawa nıaaltınıu. Wachezaji wa michezo kama hii hupata umaarufu kitaifa na kimataifa.

Hali kadhalika, wachezaji weng wameweza kujiendeleza kiuchumi kutokana na fedha wanazopata kutoka michezoni.

Wengine hujipatia ınarafiki wa kudumu kupitia michezo hii. Wapo hata waliowahi kufunga ndoa na waja kutoka mataifa mengine! Ni muhimu kukumbuka kwamba ule wakati ambao michezo ilihusishwa na watu wasiojiweza kimasoıno umetupa kisogo. Ni muhimu kuanza kutambua na kuvituınia vipawa vyetu kwa njia ifaayo. Wale walio na vipawa katika michezo nao watalıadhari dhidi ya kuchukua muda wao wote katika michezo na kuyapuuza masomo.

Elimu ndiyo itakayokuwezesha kutumia mtaji unaopata michezoni kwa njia inayokufaidi wewe na jamii yako. 31. Katika aya ya kwanza mwandishi:

A. Awaza kuwa msomaji atakuwa inwanamichezo kijijini.

B.✔ Ana hakika kwamba msomaji aliwahi kuhieza.

C. Ana tumaini kwamba msomaji anaweza kucheza.

D. Anajua kwamba msomaji alichezea sliule.

32. Aya ya kwanza inaonyesha hali ya watu:

A. Kufanya mambo yasiyo na faida kwao.

B. Kutotambua lengo la michezo shuleni.

C. Kutozinpatia ubora wa kuepuka nıajuto.

D.✔ Kujihusisha na shughuli bila kuwazia ınaana yake.

33. Kulingana na aya ya pili, Kibe:

A. Humpa mtu hamu ya kushirikiana na familia.

B. Hurahisisha juhudi za kuwatafutia wengine suluhisho.

C. Humfanya mtu kufahamu jinsi wengine wanavyohepa.

D.✔ Humwezesha mtu kujivunia uwezo wake katika jambo.

34. Mwandishi:

A. Alijithamini zaidi kwa kufahamu kufanana kwa uwezo wa tîara na wa kipungu.

B.✔ Alijiamini zaidi kwa kutambua amechangia katika mafanikio yake.

C. Alijasirika zaidi kwa kung’amua kwamba amehusika katika kuiboresha dunia.

D. Alipumbazika zaidi kwa kufikia nıbingu wakiwa watoto.

35. Chagua jibu ambalo si sahihi kulingana na aya ya tatu.

A.✔ Mtn anapoiga yafanywayo na wengine huwa na ıuafanikio mengi shuleni.

B. Wanajamii wanaweza kurekebisha tabia hata katika shughuli za kawaida.

C. Tuyafanyayo tukiwa watoto baadaye huathiri mazoea yetu.

D. kufanikiwa katika jambo ni njia ya iiujenga tabia.

36. Kifungu kimeonyesha kwamba, ilikuwa kawaida kwa:

A. Nyumba kuwa karibu na nyingine.

B. Makundi kuandikiana vitanza ndimi.

C. ✔ Watoto kujunıuika pamoja katika shughuli.

D. Vikao kukumbushana kuhrısu kushindwa.

37. Chagua umuhimi: wa michezo kwa mujibu wa aya ya nne.

A. Huleta ubunifu, hustawisha utani.

B.✔ Huimarisha utamkaji wa sauti, huboresha uważaji.

C. Hukuza ushirikiano wa kijamii, huokoa wakati.

D. Huliwaza washiriki, liuwatunibuiza wanaosimulia hadithi.

38. Kwa mujibu wa kifungu:

A.✔ Michezo husaidia mwili kunııfaika kwa lishe upatayo.

B. Mbio za kuzunguka huifanya akili ya mtu kufikiri vyema.

C. Urafiki wa dhati hupatikana baada ya michezo.

D. Waogeleaji hupata sifa wanapoogelea ng’ambo.

39. Kulingana na aya ya mwisho elimu:

A.✔ Humpa mtu stadi za kutumia alichofanikiwa na kuinua jamii.

B. Humpa mtu fursa ya kujua namna ya kupanga wakati ili kuimarisha utendakazi.

C. Humwezesha mtu kufahamu nafasi aliyo nayo.

D. Humwezesha mtu kutambua faida ya vipawa.

40. Maana ya umetupa kisogo ni

A. Umepuuzwa

B. Umesahaulika

C.✔ Umepita

D. Umebadili

Baridi na mzizimo vilishindana kuipiga pambaja ngozi yangu laini.

Nilitazama huku na huko kuona iwapo nitamwona binadamu yeyote niliyemfahamu katika uwanja huu wa ndege ulioshiba ukatapika watu na shughuli. Woga wa ajabu ulinikumbatia.

Moyo wangu ulianza kunidhihaki na kunihukumu kwa kuiacha nchi na watu niliowajua na kujitoma katika ulimwengu wenye kadhia nisizokuwa na mwao nazo. Hata nilipokuwa natunga macho mbele kuona iwapo mwajiri wangu huyu atawasili, maswali kikwi yaliivamia akili yangu. “Kipi kilichokufanya kuiacha familia yako ukiwa mkembe na kuukimbilia mji? Je, ungekaa kijijini mwako Mama Kedi angekutuma huku ughaibuni kuja kuifanyia kazi binadamu usiyehusiana naye kwa damu wala usaha?” Hapo Iwapo nilijipurukusha kuyajibu maswali haya akilini mwangu, nikayarudisha mawazo yangu nyuma na kuileta picha ya maisha yangu mbele ya macho yangu.

Nilikumbuka asubuhi moja mbichi katika kijiji chetu cha Tugawane. Siku moja niliwaona wazee watatu wamewasili kwenı. Ilikuwa siku ya tano baada ya mazishi ya mama yangu ambaye ndiye mzazi wa pekee niliyemfahamu. Baba yangu nasikia alikuwa amefariki miaka ninne kabla ya kifo cha mama kwa ugonjwa ule ule uliomuua mama. Wazee hawa waliniambia kuwa mimi na mnuna wangu tulikuwa mayatima, hivyo nilihitajika kwenda kulelewa na mmoja kati ya ndugu za baba. Nilijaribu kupinga, nikisema kwamba nıngeweza kuislli katika nyumba ya wazazi wangu tukitunzwa na dada yake baba lakini wakakataa katakata. Nakurnbuka jinsi ndimi na ndugu yangu Tunu tulivyokumbatiana, machozi ya ukiwa yakitiririka.

Tuikusanya virago vyetu na kuondoka; kila mmoja anaelekea njia yake. Mimi niliandamana na baba mdogo, naye ndugu yangu na baba mkubwa.

Maisha kwa baba mdogo yalikuwa mama ya mtoto mdogo aliyekosa titi la mama na kulazmika kııanawa la mbwa.

Vicheko nilivyokuwa nilnezoea kwetu viliyeyuka. Kwa baba mdogo hakuwa na nafasi ya wasichana kwenda shule. Walilelewa ili wakipevuka kidogo waozwe kwa wazee ambao walikuwa tayari kutoa fungu kubwa la mahali.

Binamu zangu hawakujali wala kupinga hali hii. Hata hivyo, mimi binafsi niliishi kwa hamaniko kuu. Nilimwomba Mungu kila mara asinijalie kukua. Ingawa sikudiriki kuhudhuria shule nikiwa kwa baba mdogo niliiona hali hii kuwa bora kuliko kuozıva kwa mzee. Jioni moja ya kipupwe ilishhudia mabadiliko makubwa katika maisha yangu. Jioni hiyo niliirsikia baba mkubwa na baba mdogo wakijadiliana kuhusu namna walivyogawana mashamba na mali ya wazazi wetu.

Lililonislıtua zaidi ni kusikia baba mdogo akisema kwamba tayari pametokea mzee ambaye amekuja kuniposa.

Usiku huo huo niliamua kuwa kwa baba mdogo lıakuniweki tena. Alfajiri na mapema ilinipata kwenye baraste kuu, nikiabiri matwana kutokomea jijini.

Ya ndugu yangu mdogo siyajui hadi sasa. Msomaji, hata ninapokuhadithia haya, machozi yananitiririka nikikumbuka nanuıa nilivyojitoma kwenye mitaa ya jiji na kuanza kung’ang’ania makombo kwenye majaa na watoto wengine ambao walidai kuwa waliondoka kwao baada ya kuchoshwa na sheria kali za wazazi wao. Msomaji, sikwambii ni siku ngapi nililala njaa, na ngapi niliuweka ubavu kwenye vijia vilivyokuwa katikati ya majengo, roho mkononi nikichelea kutendewa unyama.

Hali hii, pamoja na kutokuwa na ınsukumo wa kurudi uyuma nilikotoka ndizo zilizonisukuına kulikubali ombi la Bi Kedi la kunisafirisha milli na wasichana wengine watauo kufanya kazi kama vijakazi katika nchi hii ambayo imebaidika na kwetu kama ardhi na mbingu.

Siijui vipi mtoto wa umri wa miaka kumi na mitano anatarajiwa kuimudu kazi hii. Lakini ni maji ambayo nimeyavulia nguo.

41. Kulingana na aya ya kwanza:

A. Msiınulizi alijuta kwa sababu hakııkutana na aınjuaye.

B.✔ Hali ngeni iliyomzunguka Msimulizi ilimtia wasiwasi.

C. Nchi aliyohamia ina ınatukio yaliyomshangaza Msimulizi.

D. Shughuli nyingi uwanjani zililntia huzuni Msimulizi.

42. Aya ya tatu iınebainisha kwamba:

A. Msiınulizi hakujııa habari za baba yake.

B. Walio na ınayatiına walijitolea kumlea Msimulizi na nduguye.

C.✔ Msimulizi alihofia kıılelewa na arni zake.

D. Dada yake baba aliwalea vyema Msimulizi na ndugu yake.

43. Chagua athari za uyatima kwa mujibu wa kufungu.

A.✔ Kuutengana na familia, kudhoofika kwa malezi.

B. Wasiwasi, udanganyifu.

C. Kıısafiri nchi jirani, kubaguliwa shuleni.

D. Umaskini, kujidharau.

44. Chagua jibu ambalo si sahihi kulingana na aya ya nne.

A. Baba mdogo alimnyima Msimulizi mengi aliyoyapata kwao.

B.✔ Wasichana waliokoınaa ndio waliohitaji mahari nyingi.

C. Watoto wa baba mdogo waliridhika taa hali yao.

D. Jamii ya Msimulizi inaendeleza ubaguzi eva kijinsia.

45. Ingawa sikudiriki kuhudhuria shule nikiıva kwa baba mdogo,

niliiona hali hii kuwa bora kuliko kuozwa kwa mzee.

Andika methali inayoweza kujumııisha ujumbe wa ınaneno maya.

A. Mwacha kiwi hanacho na cheına kihıpotele.

B. Kenda fumbata si kuıni nenda indi.

C.✔ Heri nusu ya shari kuliko shari kamili.

D. Bııra yangu sibadili na rehani.

46. Kwa nini hasa atni za Msimulizi walitaka kuwalea? Waliongozwa na

A.✔ tamaa ya kunıiliki mali ya wazazi wa Msimulizi

B. hamu ya kujua urithi wazazi wa Msinıulizi

C. haja ya hupata ınahari baada ya binti kuozwa

D. tumaini la kufaidi kwa watoto wakimaliza shule.

47. Chagua changamoto zinazowakabili watoto wa mitaani kulingana na aya ya mwisho.

A. Uhaba wa chakula, kutopata washîrika.

B. Kudhibitiwa na wazazi, kushindana kwenye majaa.

C. Malazi duni, kutafuta walezi.

D.✔ Ukosefu wa usalama, kunyanyaswa kimapenzi.

48.Kulingana na aya ya mwisho:

A. Mazingira duni ya rnjini yalinafanya Bi Kedi aanzishe biashara ya vijakazi.

B. Kııwachukia wasichatıa ktlliwafanya kukubali kuwa vijakazi.

C.✔ Msiıuulizi yı tayari kukabiliaha na hali n3ınnu anayotazanıia.

D. Umı‘i tınaınfanya Msinuılizi kuogopa ng’ambo.

49. Kauli,‘maswali kikwi yalivamia akili yangu imetumia tamathali gani ya usemi?

A. Nahau.

B.✔ Tashihisi.

C. Sitiari.

D. Majazi.

50. Kuwa roho mkononi ni

A. Kupata hisia tele.

B. Kuonyesha tuhuma kuu.

C.✔ Kuwa na woga mwingi.

D. Kujawa na huzuni nyingi.