KPSEA 2022 Exams Past Papers(Grade 6)- Kiswahili

KPSEA 2022 Exams Past Papers(Grade 6)- Kiswahili

November 2022 – Muda Saa 1

MASWALI

Swali la 1 hadi la 5.
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

(Babu ameketi chini ya mti akisoma gazeti. Analiweka gazeti kando anapomwona Muli)
Muli: (akimsogelea Babu) Shikamoo Babu?
Babu: (kwa tabasamu) Marahaba mjukuu wangu! Habari za shule?
Muli: Njema babu! (kimya) Babu, nikwambie kitu?
Babu: Naam, niambie mjukuu wangu.
Muli: Wenzangu walinichagua kuwa kiranja wa darasa.
Babu: Hongera! Jambo zuri.
Muli: (akijikuna kichwa) Lakini Babu, sijui ninastahili kufanya nini ili niwe kiongozi bora.
Babu: Aha! Muli, sikiliza, ili kuwa kiongozi bora unastahili kuwa na maadili.
Muli: Ooh! Maadili…
Babu: Naam mjukuu wangu. Unaweza kuonyesha maadili kwa namna mbalimbali. Kwanza uwahudumie wenzako bila kuwabagua.
Muli: Kweli Babu, ninafikiria pia ninastahili kuwaonyesha upendo.
Babu: Ndiyo Muli. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwajali na kuwasaidia wenzako.
Muli: Kweli Babu! Ninaona kwamba heshima, umoja na ushirikiano pia ni mambo muhimu.
Babu: Haswa! Heshima si utumwa. Je, unaweza kuonyesha heshima kwa njia gani?
Muli: (Kwa ujasiri) Kwa kuwaamkua wote na kusikiliza wanayoyasema.
Babu: Vyema! Unastahili pia kuwa mwaminifu. Tunaonyesha uaminifu kwa kusema ukweli na kufanya mambo inavyostahili.
Muli: Asante babu! Hakika umenifunza mengi.

 1. Muli alipoulizwa na babu kuhusu habari za shule, alimjibu
  1. Naam
  2. Njema
  3. Shikamoo
  4. Marahaba
 2. Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi halionyeshi adabu?
  1. Karibu
  2. Naam
  3. Asante
  4. Kweli
 3. Ni jibu lipi linaloonyesha maadili ambayo Babu alimfunza Muli?
  1. Kuhudumia, kuheshimu na kusikiliza. 
  2. Kuamkua, kusikiliza na kujali.
  3. Kujali, kusaidia na kuwa mwaminifu.
  4. Kuwa na heshima, kushirikiana na kusaidia.
 4. Unafikiri Muli atafanya nini baada ya kumuaga Babu?
  1. Atafurahia kuwa kiongozi shuleni.
  2. Atazingatia mawaidha ya babu.
  3. Atawaeleza wenzake kuhusu alivyokutana na babu.
  4. Atawapongeza wenzake kwa kumchagua kuwa kiranja
 5. Neno maadili limetumika katika mazungumzo maana yake ni
  1. Mienendo mizuri inayofaa kuzingatiwa na mtu.
  2. Maonyo ambayo hutolewa mtu anapokosea. 
  3. Matendo ambayo mtu huwafanyia wenzake.
  4. Mitindo mipya inayofuatwa na mtu.

Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Sungura alirauka kabla ya jua kuchomoza. Alianza safari ya kwenda kumtembelea shangazi yake. Njiani alipanda milima na kuvuka mabonde. Jua lilipochomoza, aligundua kuwa alikuwa ametembea sana ila hakuwa amefika kwa shangazi yake. Alikuwa anaelekea kusini badala ya kaskazini. Kumbe alikuwa amepotea njia! “Nitafanya nini? Nimepotea njia,” Sungura alijisemea kwa sauti.
“Nitakusaidia,” alisema Kobe aliyekuwa kichakani, hapo karibu.
“Asante sana Kobe. Sikuwa nimekuona. Tafadhali nisaidie.” Sungura alimwomba Kobe.
“Unakwenda upande gani?” Kobe alimuuliza Sungura.
“Naelekea kaskazini, anakoishi shangazi yangu,” Sungura alimjibu Kobe.
“Jua huchomoza upande wa Mashariki wa dira kila asubuhi. Ukitaka kwenda Kaskazini, simama kisha unyooshe mikono yako juu. Mkono wa kulia uuelekeze kunakotoka jua. Huko ndiko Mashariki. Nao mkono wa kushoto uuelekeze upande huo mwingine. Huko ndiko Magharibi,” Kobe alimweleza Sungura huku akimwonyesha kwa vitendo.
“Kwa hivyo uso wangu utakuwa unaangalia Kaskazini huku mgongo wangu ukiwa upande wa Kusini” Sungura alisema kwa furaha.
“Wewe ni mwanafunzi mzuri. Unaelewa haraka. Umelenga ndipo,” Kobe alimwambia Sungura kwa bashasha.
“Undugu ni kufaana. Asante sana Kobe,”
Sungura aligeuka akarudi hadi kwake ili kuanza safari upya.

 1. Nyumbani kwa Shangazi kulikuwa upande gani kutoka kwa Sungura?
  1. Mashariki
  2. Magharibi
  3. Kaskazini
  4. Kusini
 2. Kwa nini Sungura aliamka mapema? Ili
  1. apande milima na kuvuka mabonde. 
  2. aone jua likichomoza.
  3. akutane na Kobe njiani.
  4. aende kumtembelea Shangazi.
 3. Kobe anawajali wengine. Chagua jibu lin- aloonyesha sifa hii ya Kobe.
  1. Alimwelekeza Sungura alikokuwa akienda. 
  2. Anamsikiliza Sungura akizungumza.
  3. Alikubali zawadi alizopewa na Shangazi.
  4. Alifikiria Sungura alikuwa mwanafunzi mwerevu.
 4. Chagua jibu lenye neno ambalo Shangazi angetumia kumwita Sungura.
  1. Binamu
  2. Mpwa
  3. Ndugu
  4. Ami

Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Shule ya msingi ya Faulu huwa na siku tatu za michezo katika kila juma. Wanafunzi wa Gredi ya Sita wamegawanywa katika vikundi vinne kama ifuatavyo: Simba Kifaru Chui Ndovu
Kila kikundi hushiriki katika michezo tofauti kila juma. Tazama jedwali la juma hili kisha ujibu maswali.

VIKUNDI JUMATATU  JUMATANO IJUMAA 
 Simba Kandanda  Netiboli Riadha
 Kifaru Riadha Uogeleaji Kandanda
 Chui Netiboli Riadha Uogeleaji
 Ndovu Uogeleaji Kandanda Netiboli
 1. Ni kikundi kipi hakikushiriki kandanda?
  1. Simba
  2. Chui
  3. Kifaru
  4. Ndovu
 2. Ni kikundi kipi hakikushiriki uogeleaji?
  1. Ndovu
  2. Kifaru
  3. Chui
  4. Simba
 3. Ni kikundi kipi hakikushiriki riadha?
  1. Simba
  2. Chui
  3. Ndovu
  4. Kifaru

Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Je, unajua kupika ugali? Kupika ugali ni rahisi. Kwanza, unahitaji unga wa mahindi, maji, sufuria, mwiko na jiko la kupikia lenye moto. Anza kwa kupima kiasi cha maji unayohitaji na kuyatia kwenye sufuria safi. Ibandike sufuria hiyo kwenye jiko. Funika sufuria ili uyapatie maji muda yachemke. Chukua unga kisha uutie kidogo kidogo ndani ya maji yanayochemka, huku ukikoroga kwa mwiko. Ongeza unga kulingana na unavyotaka ugali wako uwe. Kama unataka ugali mgumu, basi endelea kuongeza unga. Funika ugali wako, kisha upunguze moto jikoni ili ugali uive polepole.
Unaweza kuandaa ugali kwa vitoweo vya aina mbalimbali. Kuna wale wanaopenda kula ugali kwa maziwa yaliyoganda na mboga za kienyeji kama vile mchicha. Wengine hula ugali kwa samaki au nyama. Mimi napenda kula ugali kwa dagaa na kachumbari. Je, wewe unapenda kula ugali kwa kitoweo gani?

 1. Wewe unajiandaa kupika ugali.
  Chagua jibu linaloonyesha hatua ya kwanza utakayozingatia
  1. Kuwa na vitu utakavyohitaji kupika ugali.
  2. Kuinjika sufuria yenye maji jikoni. 
  3. Kuchukua mwiko na kuanza kukoroga.
  4. Kuwa na kitoweo ambacho unahitaji.
 2. Unampikia nyanya kitoweo cha kuliwa kwa ugali.
  Chagua jibu linaloonyesha kitoweo chenye lishe bora.
  1. Nyama na dagaa.
  2. Kabeji na sukumawiki.
  3. Samaki na mboga ya mchicha.
  4. Maziwa na maharagwe.
 3. Chagua jibu sahihi.
  Mchicha huupatia mwili vitamini, ugali huupatia mwili …………………………
  1. protini.
  2. madini.
  3. kinga.
  4. wanga.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Kanini 16                         katika michezo mbalimbali tukiwa shuleni. Mchezo 17                    alipenda zaidi ni netiboli. 18                    na timu ya mchezo wa netiboli 19                   alipoingia darasa la tano. Kanini alitia bidii kwenye mchezo huu na kuiletea timu yake ushindi. Alifahamu kuwa 20                     .

 1. alishirikia
 2. alishiriki
 3. alishirikisha
 4. alishirikiwa

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

 1. Wanafunzi wana nidhamu, …………………………¬†huheshimu walimu.
  1. wao
  2. wewe
  3. yeye
  4. nyinyi
 2. Tunasema, wingu ni kwa nzige. Tutasema, ………………………………..ni kwa matunda.
  1. kitia
  2. pakacha
  3. bunda
  4. robota
 3. Chagua wingi wa:
  Fundi yule hodari amejenga ukuta mrefu.
  1. Mafundi wale hodari wamejenga kuta ndefu.
  2. Fundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
  3. Mafundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
  4. Fundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
 4. Kimeto alimsaidia Kamaa kuchora picha.
  Kamaa alikuwa ameumia mkono. Kwa hivyo, Kimeto
  1. alimchoresha Kamaa picha.
  2. alimchorea Kamaa picha.
  3. alichoreshwa picha na Kamaa..
  4. alichoreshea Kamaa picha.
 5. Ni sentensi ipi sahihi?
  1. Palipo na rutuba panafaa kwa kilimo.
  2. Palipo na rutuba kunafaa kwa kilimo.
  3. Mlimo na rutuba panafaa kwa kilimo.
  4. Mlimo na rutuba kunafaa kwa kilimo..
 6. Ni sentensi ipi iliyoafikishwa vyema?
  1. Neema amefika: kwetu leo asubuhi..
  2. Mwachia amenunua machungwa, maembe na papai.
  3. Je, umeandika barua ya kuomba msamaha.
  4. Salaale Kalama amefunga bao lingine.
 7. Chagua ukubwa wa sentensi ifuatayo: Mlango wa nyumba yake unapendeza.
  1. Lango la jumba lake linapendeza.
  2. Mlango wa jumba lake linapendeza.
  3. Lango la nyumba yake linapendeza.
  4. Mlango wa nyumba yake linapendeza.
 8. Chagua jibu lisilo sahihi.
  1. Tita la kuni.
  2. Thureya ya nyota.
  3. Kicha cha funguo.
  4. Kilinge cha wanariadha.
 9. Tunastahili kupiga chafya kwenye kiwiko cha mkono. Kupiga chafya ni
  1. kuchemua.
  2. kukohoa.
  3. kutema.
  4. kupenga.
 10. Simon ni wembe masomoni. Kauli hii ina maana kuwa Simon ni:
  1. mwenye subira.
  2. jasiri.
  3. mwenye bidii.
  4. mwerevu.