2012 KCPE Kiswahili Past Paper-Free KCPE Past Papers with Answers.

Kenya National Examinations Council

K.C.P.E 2012

Kiswahili

Sehemu ya kwanza:

Lugha

Muda: Saa 1 dakika 40

DAY 2

Wednesday : 14/11/2012

Maagizo kwa watahiniwa

Soma kwa makini maagizo yafuatayo:

1. Umepewa kijitabu hiki cha maswali na karatasi ya kujibia. Kijimbu hiki kina maswali 50.

2. Ukiisha kuchaguajibu lako, lionyeshe katika karatasi ya majibu na wala sio katika kijitabu hiki cha maswali.

Jinsi ya kutumia karatasi la majibu

3. Tumia penseli ya kawaida.

4. Hakikisha ya kwamba umeandika yafuatayo katika karatasi ya majibu:

Namba yako ya mtihani

Jina lako

Jina lako la shule:

5. Kwa kuchora kistari katika visanduku vyenye namba zinazokuhusu, onyesha namba yako kamili ya mtihani (yaani namba ya shule. na zile namba tam za mtahiniwa) kaiika sehemu iliyolengwa mwanzo wa karatasi ya majibu.

6. Usitie alama zozote nje ya visanduku.

7. lweke safi karatasi yako ya majibu na usiikunje.

8. Kwa kila swali 1 — 50 umepewa majibu manne. Majibu hayo yameonyeshwa kwa herufi A, B, C, D. Ni jibu MOJA tu kati ya hayo manne ambalo ni sahihi. Chagua jibu hilo.

9. Kwenye karatasi ya majibu, jibu sahihi lionyeshwe kwa kuchora kistari katika kisanduku chenye herufi uliyochagua kuwa ndilo jibu.

Mfano:

Katika kijitabu cha maswali:

21 . Chaguajibu lenye ala za muziki pekee.

A. filimbi, udi, mvukuto, chapuo

B. njuga, tari, kinubi, fidla

C. harimuni, marimba. msondo, maleba

D. siwa. zeze, upatu, nembo.

Jibu sahihi ni B

Katika karatasi ya majibu:

1. [A] [B] [C] [D] 11. [A] [B] [C] [D] 21. [A] [B] [C] [D] 31. [A] [B] [C] [D] 41.[A] [B] [C] [D]

Katika visanduku vinavyoonyesha majibu ya swali namba 21, kisanduku chenye herufi B ndicho kilichochorwa kistari.

10. Chora kistari chako vizuri. Kislari chako kiwe cheusi nu kisijitokeze nje ya kisanduku.

11. Kwa kila swali. chom kistari katika kisanduku kimoja tu kati ya visanduku vinne ulivyopewa.

Kijitabu hiki cha maswali kina kurasa 7 zilizopigwa chapa.

Maswali 1 mpaka 15.

Soma vifungu vifimlavyn. Vina nafasi 1 hadi 15. Umepewu majibu manne hapo. Chaguajibu lifaulo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kiswahili ni mojawapo ya lugha _1_ wazungumzaji wengi. Lugha ya Kiswahili _2 zama za ukoloni 3_ Waafrika dhidi ya wakoloni. Hatua ya kukifanya Kiswahili lugha rasmi nchini Kenya _4_ hadhi ya lugha husika. 5_ hapo awali, tunatarajia Kiswahili kutumiwa 6- na Kiingereza katika shughuli za kiofisi. Hata hivyo, 7- patakuwa na haja ya kutafsiriwa kwa makala mengi kwa Kiswahili.

1 . A. yenye

B. zenye

C. wenye

D. chenye

2. A. ingekuwa imetumiwa

B. ilikuwa imetumiwa

C. ingekuwa ikitumiwa

D.ilikuwa ikitumiwa

3. A. kuwatambulisha na kuwaunganisha

B. kuwahamasisha na kuwalinganisha

C. kuwadumisha na kuwajenga

D. kuwastawisha na kuwalenga

4. A. imeieneza

B. imcitia fora

C. imeikweza

D. imeivika kjlemba 5. A. Licha ya

B. Bighairi ya

C. Mbali na

D. Kinnyume na 6. A. mtawalia

B. mkabala

C. sadakta

D. sambamba

7. A. hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe

B. hakuna marefu yasiyokuwa na ncha

C. hakuna bamvua lisilo usubi

D. hakuna kubwa lisoshindwa

Mtoto ana haki 8- . Anastahili 9- vizuri ili kuifaa jamii 10- . Tabia ya mtoto 11- na jamii, hivyo tunaweza kudai kuwa mtoto ni zao la jamii. 12-, mtoto ana haki ya lishe bora 13- nguvu yaani, 14-, na kumwezesha kujikinga na maradhi kama vile 15- . Ugonjwa huu husababishwa na kula chakula arnbacho kina upungufu wa viinilishe

8. A. maradufu

B. akali

C. anuwai

D. maridhia

9. A. kukidhiwa

B. kutunikiwa

C. kuengaengwa

D. kutunzwa

10. A. yetu

B. yake

C. yangu

D. yenu

11. A. huathirika

B. huathiria

C. huathiriana

D. huathiriwa

12. A. Aidha

B. aghalabu

C. yamkini

D. pengine

13. A. litakaompa

B. itakapompa

C. litakalompa

D. itakayompa

14. A. azma

B. ilhamu

C. siha

D. hima

15. A. safura

B. utapiamlo

C. surua

D. tetekuwanga

Kutoka swali In 16 mpaka 30. chagua jibu lililo sahihi.

16. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi? (i) muhibu (ii) muhtasari (iii) muhali (iv) muhula A. (iii), (ii), (i), (iv)

B. (iii), (i),(ii), (iv)

C. (iv), (i), (ii), (iii)

D. (iv), (ii), (i), (iii).

17. Umoja wa: “Nywele zao ndefu ziliwavutia,“ ni:

A. Nywele yake ndefu iliwavutia.

B. Nywele zake ndefu zilimvutia.

C. Unywele wake mrefu uliwavutia.

D. Unywele wake mrefil ulimvutia.

18. Chaguajibu lenye nomino zilizo kalika ngeli ya I-I pekee.

A. kahawa, fedha:

B. chumvi, chupa;

C. mali, chai;

D. sukari, mvua.

19. Ni jibu lipi lenye maelezo sahihi?

A. Muundi ni sehemu ya mkono kuanzia begani hadi kwenye kiwiko.

B. Kitengele ni sehemu ya mwisho ya mkono ycnye vidole.

C. Nyonga ni schemu yajuu ya kiuno.

D. Paji ni sehemu yajuu ya kichwa.

20. Hisani ni kwa wcma na kunadi ni kwa: A. kuuza

B. kutangaza:

C. kusambaza;

D. kuchuuza.

21. Chagua kinyume cha: ‘Wageni waliwasili kabla ya eropleni kupaa.’

A. Wenyeji waliondoka baada ya eropleni kutua.

B. Wenyeji waliondoka kabla ya eropleni kutua.

C. Wageni waliondoka kabla ya eropleni kutua.

D. Wageni waliondoka baada ya eropleni kutua.

22. Tikiti. limau na fenesi ni matunda ilhali Wimbi, mahindi na mtama ni:

A. mitil

B. vyakula;

C. nafaka;

D. mbegu.

23. 6/9 kwa maneno ni:

A. sudusi sita;

B. tusui sita;

C. tusui tisa;

D. sudusi tisa.

24. Kukanusha kwa: “Nyungu iliyonunuliwa iliuzwa tena,“ ni:

A. Nyungu iliyonunuliwa haijauzwa tena.

B. Nyungu iliyonunuliwa haikuuzwa tena.

C. Nyungu isiyonunuliwa haijauzwa tena.

D. Nyungu isiyonunuliwa haikuuzwa tena.

25. Ni jibu lipi ambalo si aina ya shairi’? A. kibwagizo;

B. tathlitha:

C. ngonjera;

D. tarbia.

26. Onyesha sentensi yenye kielezi cha mahali.

A. Hukimbizana mara kwa mara.

B. Wanafimzi watafuzu mwakani.

C. Kambo alisafiri kwa gari.

D. Tulielekezwa pembezoni.

27. Kiambishi ‘ka’ katika sentensi: “Alienda shuleni akasome Kiswahili;” kinaonyesha:

A. kufuatana kwa malukio;

B. kulazimika;

C. kusudi;

D. kutegemeana kwa matendo.

28. Chagua kundi Iinaloonyesha kitenzi kilichoundwa kutokana na kivumishi.

A. Mvumilivu – uvumilivu;

B. Mwaminifu – aminika;

C. Mapishi – pikika

D. Wacheshi – ucheshi.

29. Kilara ni upanga mwembamba wa kuunguzea gwaridc. Kitara vile vile ni:

A. sehemu iliyotengenezwa kukaushia mbegu:

B. chombo kitumiwacho kufungia mlango

C. nazi changa ambayo haijawa dafu;

D. sehemu inayopandwa mimea au miche.

30. Chagua sentensi ambayo imetumia ‘na’ kama kiunganishi.

A. Wafanyakazi wore wameitwa na nokoa shambani.

B. Wafanyakazi waliokuja wanajulikana na nokoa wao.

C. Wafanyakazi na nokoa wao wanalima shamba.

D. Wafanyakazi walikuwa na matumaini ya kumwona nokoa.

Soma kifungu kifizatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Kuna aina mbili kuu za misitu. lpo ile ya kiasili kama vile Msitu wa Karura na Msitu wa Mau. Hali kadhalika, ipo misitu ya kupandwa kama ile ya Kinale na Webuye. Misitu ni hazina kubwa kwa jamii yoyote ile. Kila mwanajamii anapaswa kujivunia misitu.

Misilu husheheni miti ya aina nyingi ambayo, pamoja na kuwa makazi ya wanyama, hutoa vyakula kama vile matunda na majani ambayo huwafaidi binadamu na viumbe wengine. Bila misitu binadamu nu wanyama wangeangamia.

Misitu ni kivutio cha watalii. Watalii kutoka ndani na nje ya nchi huzuru misitu na mbuga mbalimbali za wanyama kuajabia uzuri wake. Watalii hawa hulipa fedha za kigeni ambazo hutumiwa kuanzishia miradi ya kiuchumi kama vile kustawisha miundomsingi.

Fauka ya hayo, misitu husafisha hewa na kurembesha mandhari wanamoishi binadamu. Rangi ya kijani kibichi na maua yenye rangi tofauzitofauti huyafanya mazingira kupendeza hata yakitazamwa kwa mbali. Mandhari yasiyo na miti hayakosi urembo tu, bali huwa wazi kiasi kwamba hata mapaa ya majengo yaliyo hapo wakati mwingine hupeperushwa na upepo mkali. Vipindi virefu vya jua huwanyima viumbe starehe na huweza kusababisha saratani ya ngozi kwa binadamu. Miti hufanya vivuli ambavyo huwakinga watu na wanyama dhidi ya miale ya jua. Isitoshe, si ajabu kuwa mahali ambapo pana miti mingi kwa kawaida hupala mvua hata wakati usio wa majira ya mvua kwingineko.

Sekta ya tiba imefaidika si haba kutokana na miti. Matabibu wa kienyeji na hata wa kisasa hutumia mizizi, majani na magome ya miti kutengenezea dawa. Miti kama vile mwarubaini hutibu magonjwa mengi. Hivi sasa magonjwa kama vile bolisukari , shinikizo la damu na ugonjwa wa figo yameweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa zinazotokana na miti. lnasemekana kuwa hata nyoka humtibu nyoka mwenzake kwa majani!

Miti hutumiwa viwandani kutengenezea bidhaa kama vile karatasi na samani. Viwanda hivi hutoa ajira kwa maelfu ya raia, hivyo kupunguza makali ya uhaba wa nafasi za kazi nchini. Ni wazi kuwa uhifadhi wa misitu una manufaa tumbi nzima kwa binadamu. Hata hivyo. binadamu mwenyewe ndiye anayeiangamiza misitu yenyewe. Watu wenye mate ya fisi wamekata miti kiholela kwa ajili ya kupata kuni na kuchomea makaa ya kuuza. La kusikitisha ni kwamba watu hawa hawadiriki kupanda miti mingine kufidia ile waliyoikata. Wengine, kwa kutojua wanajipalia makaa, hupanda miti ambayo inakausha vyanzo vya maji na kuchangia kuenea kwa kasi kwa jangwa. Hali kadhalika, wapo warina asali ambao katika juhudi zao za kurina husababisha kuteketea kwa misitu.

Kifungu cha katiba kinachohusu mazingira na mali ya asili kinasisitiza suala la uhifadhi wa mazingira. Kila mwanajamii basi ana jukumu la kuilinda misitu na kucpuka mazoea ambayo yanaiangamiza, la sivyo tutakuwa tunajichimbia kaburi. 31. Kulingana na kifungu, mchango wa utalii kwa jumla ni: .

A. kuongeza fedha za kigeni kwenye mbuga;

B. kuboresha miundomsingi kwenye misitu;

C. kuimarisha uchumi wa nchi;

D. kuwekeza miradi ya nchi.

32. Chagua hasara za kutohifadhi misitu kwa mujibu wa kifungu. 3

A. kunyauka kwa majani, kupoteza urembo;

B. kuporomoka kwa majengo, kupoteza mvuto;

C. mahali pakavu, kuchukiza kwa mazingirzra

D. upepo mkali, kunyauka kwa maua.

33. Ni jibu lipi sahihi kulingana na kifungu? A. Dawa za kienyeji huponya kabisa magonjwa mengi sugu.

B. Kuhifadhi misitu kunaweza kuchangia kuongezeka kwa nafasi za kazi.

C. Mahali penye miti mingi hupata mvua inayotegemcwa kila mara.

D. Kuwa na vipindi vya jua kali kunawcza kusababisha saratani.

34. Kifungu kinasema kuwa miti hummiwa:

A. kutcngenezea kawi na kuwasetiri viumbe:

B. kuunda samani na kuhifadhi maji:

C. kusafishia hewa na kufanikisha majengo

D. kuvuta mvua na kuburudisha viumbe.

35. Maana ya methali, “Mwiba wa kujichoma hauambiwi pole.“ imedhihirika katika kifungu kwa vile:

A. Watu ndio wanaojisababishia hali mbaya ya ukame kwa kupuuza umuhimu wa miti.

B. Watu ndio wanaojisababishia hali mbaya ya kiangazi kwa kupuuza umuhimu wa misitu.

C. Watu ndio wanaojikaushia visima kwa kupanda miti isiyofaa.

D. watuu ndio wanaojichomea misitu kwa kurina pasipostahili.

36. Mwandishi anaonyesha kuwa kichocheo kikuu cha kukala miti ni:

A. kuwa na haja ya kuuza makaa;

B. kuwa na hamu ya kupata asali;

C. kuwa na tamaa ya mali;

D. kuwa na mahitaji ya kuni.

37. Nijibu Iipi ambalo si sahihi kulingana na aya ya nane?

A. Ukataji miti unapaswa kuandamana na upandaji miti upya.

Shughuli yenyc faida huweza kuishia kuwa janga.

C. Ukosefu wa maarifa unawcza kusababisha hasara.

D. Jaribio la kupanda miti linastahili kuepuka panapotolewa maji.

38. Kulingana na aya ya mwisho: A. Mazingira huhifadhiwa kupitia kwa kifungu cha katiba.

B. Mwanajamii hujiletea majuto kwa kutoepuka mienendo isiyokubalika.

C. Mazingira huharibiwa na hulka zisizofa za binadamu.

D. Mwanajamii anastahili kufuata mshawasha wa katiba.

39. Kwa mujibu wa taarifa, ‘yameweza kudhibitiwa’, ina maana:

A. Yameweza kuondolewa;

B. Yameweza kuzuiliwa;

C. Yameweza kutibiwa yote;

D. Yamcweza kupunguzwa yote.

40. Maana ya, ‘hawadiriki’, kulingana na kifungu ni:

A. hawawahi;

B. hawaambulii;

C. hawarauki;

D. hawawazii.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Tenga alilelewa katika mazingira yaliyojaa neema, furaha na uchangamfu. Wazazi wake Bwana Mtanga na Bi. Zuhura waiikuwa wakwasi wa kutajika katika janibu hizo. si kwa mali tu bali kwa nyoyo zao zilizokuwa tayari kila mara kuwakirimu wanakijiji kwa lolote.

Bwana Mtanga na Bi. Zuhura hawakuiala maskini wakaamka matajiri. Mtanga alianza kazi kama tarishi katika Makavazi ya Umma. lngawa hii ilikuwa kazi ya kijungu jiko mekoni. Mtanga hakwenda nguu: alijitahidi kwa vyovyote vile kujinyanyua. Akajisajili kwa kozi mbalimbali za usimamizi wa makavazi na kuhilimu vyeli lofautitofauli vikiwemo stashahada na shahada katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma. Jitihada zake zikazaa matunda. Akapandishwa cheo mwaka baada ya mwingine hadi akawa msimamizi wa Makavazi ya Umma. Baadaye akaajiriwa na shirika la Mszilaha Mwckundu kama Mkrurugenzi wa Huduma za Kijamii.

Bi. Zuhura naye. baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili. alisomea taaluma ya ukulubi na baadaye kuajiriwa katika maktaba ya chuo kikuu cha Tungama. Hapa Zuhura alitambua kuwa amepata nafusi adimu ya kuulia makali ubongo wake. Akajisajili kwa kozi ya ukutubi na kuhitimu shahada ya daraja la kwanza kmika raaluma hii. Wakuu wake kazini wakavutiwa na juhudi zake na kumpandisha cheo. akawa Mkutubi Mkuu.

Wakati Bwana Mlanga na Bi. Zuhura walipokuwa wakijiendelcza kitaaluma na kiuchumi.Tenga naye alikuwa anajikulia lu kama uyoga bila mpalilizi. Nyadhifa za wazazi wakek zilimpokonya Tenga ushirika wa wazazi wake. Ile michezo yake na wazazi wake kabla ya chajio. yale maiembezi ya kila Jumapili yote yakatoweka. Baba na mama wakawa wanarudi nyumbani baada ya saa nne usiku wakiwa wametoka kwenye masomo ya kuupigia msasu ujuzi wao; Jumamosi na Jumapili wana majadiliano na wanafunzi wenzao. Nyakati nyingine wazazi wote wawili walikuwa kwenye safari za kikazi. Nyakali kama hizi Tenga angepelckwa kwa shangazi ambako angekaa na kijakazi wake kwa wiki tatu; anaenda shuleni na kumdi huko huko kwa shangazi.

Wahenga walisema kwamba, akosaye la mama hala la mbwa huamwa. Pengo la maiezi lililouchwa na wazazi wa Tenga Iilijazwa na walezi wengine. wakiwemo vijakazi . shangazi, marika. walimu. majirani na ham vibonzol Tcnga alijifunza mengi kutokana na walezi hawa. Alifunzwa namna ya kupigana miereka. kutumia ujanja kujitoa katika matalizo. kutumia maneno makali kujihamialipochokozwa na wenzake, pamoja na milindo mbalimbali ya kujinadhifisha. Mafunzo ambayo Tenga aliyapata. hasa kuloka kwa marika. yaliutia ila mwenendo na uhusiano wake nu walimu. Darasani akawa haishi kuvuruga masomo kwani kila mara angelenda kituko ili mwaiimu na wanafumi waubaini uwepo wake. Vituko hivi vilisababisha kudorora kwa alama zake. Walimu wakajaribu kuurekebisha utundu wake lakini zikawa kama juhudi za mfa-maji. Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya. Mkuu wa Idara ya Ushauri na Uelekezaji shuleni ilihidi ahusishwe. Akamhoji Tenga na kupambaukiwa kuwa vitendo vya Tenga vilikuwa na asili ambayo ilihitaji kuchunguzwa. Akampendckezea mwalimu wa darasa kuwashirikisha wazazi kalika kutafuta mbinu za kumwelekeza Tenga zaidi.

Bwana Mlanga na mkcwc Zuhura walipoamhiwa kuhusu hali ya Tenga walipigwa nu bumbuazi. Hawakuwa wameyawazia madhara ya kutoshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoio wao. Mwzilimu aliwaambia ya kwamba nusura Tenga ziingizwe na wenzake katika maxumizi ya dawa za kulevya Iakini akakataa na kusema kuwa hata babake hakujaribu kutumia kilco chochote. Wazazi walionzi haya na kujilaumu. Huta hivyo walishukuru ya kwamba walimu waliyagundua malatizo haya kabia hayajaiangziniiza familia yao.

41. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu. Bwana Mtanga na Bi. Zuhura:

A. walimlea Tenga kwa kushauriana, walikuwa mashuhuri;

B. walimlea Tenga kwa kuchangamkiana walikuwa maarufu

C. waliingiliana vyema na majirani walipenda kusaidia

D. waliingiliana vyema na walimu, walipenda kutoa.

42. Utajiri wa wazazi wa Tenga ulitokana na:

A. uwajibikaji wao katika shughuli zao;

B. kupata vyeo katika madaraja tofautitofauti;

C. kupata shahada na stashahada mbalimbali;

D. uwajibikaji wao katika taaluma zao.

43. Wazo kuu linalojilokeza katika aya ya nne ni

kwamba:

A. Jambo Iolote likifanywa bila ushirikiano

B. Jambo lolote Hkifanywa bila kipimo huweza kuleta madhara.

C. Jambo lolole likifanywa bila utulivu huweza kuleta madhara.

D. Jambo lolote likifanywa bila mtazamo huweza kuleta madhara.

44. Kifungu kinaonycsha kuwa ukosefu wa malezi bora husababisha:

A. kupigana miereka daima ili kupata maslahi;

B. kudhoofika kwa maadili;

C. kuharibu masomo darasani ili kuonekana kole;

D. kuharibika kwa urafiki

45. “Tabia ya tenga haikuwa ufa bali ukuta abao ulihitaji kujengwa upya” ina maana;

A. Tabia ya tenga ilikua imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kurekebishwa kikamilifu

B. Tabia ya tenga ilikua imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kushauriwa kikamilifu

C. tabia ya Tenga ilihitaji kushughulikiwa kikamilifu

D. tabia ya Tenga ilihitaji kutambuliwa kikamilifu

46. Kwa mujibu wa kifungu. Idara ya Ushauri Uelekezaji inasaidia katika malezi kwa

A. kuwahoji vijana na kuwaita wazazi wao:

B. kutambua malmizo ya vijana na kuonyesha mbinu za kuwashirikisha;

C. kutambua matatizo ya vijana na kuangazia mbinu za kuyasuluhisha;

D. kuwahoji vijana na kuwaambia matatizo yao.

47. Kulingana na aya ya mwisho, wazazi wa Tenga hawakujua umuhumi wa kukaa karibu na watoto wao walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu wa walezi wao walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu na mtoto wao hawakujua umuhimu wa kukaa karibu na walezi wao

48. Chagua jibu Iinaloonyesha sifa za Tenga. A. mcheshi, mwenye kupenda wazazi;

B. mwenye mapenzi ya dhati. anayelafuta kushirikishwa;

C. mchangamfu mwenye kupenda unadhifu;

D. mwenye msimamo imara, anayelafuta kutambuliwa

49. Kisawe cha, ‘hakwenda nguu.’ ni:

A. hakujitia kapuni;

B. hakujitia hamnazo;

C. hakufa mayo;

D. hakufa kikondoo.

50. Maana ya, ‘kujihami’ kwa mujibu wa kifungu ni:

A. kujitetea;

B. kujinasua:

C. kujihadhari;

D. kujuzatiti.

2012 KCPE Kiswahili Past Paper Marking Scheme/Answers

1 B

2 D

3 A

4 C

5 D

6 D

7 C

8 C

9 D

10 B

11 D

12 A

13 D

14 C

15 B

16 B

17 D

18 D

19 B

20 B

21 A

22 C

23 B

24 B

25 A

26 D

27 C

28 B

29 A

30 C

31 C

32 B

33 B

34 A

35 A

36 C

37 D

38 C

39 B

40 A

41 C

42 D

43 B

44 B

45 A

46 C

47 C

48 D

49 C

50 A