MAAGIZO
• jibu maswali maswali yote katika nafasi ulizopewa.
• Majibu lazima yaandikwe katika lugha ya Kiswahili
- UFAHAMU – ALAMA 15
Ulimwengu mzima ulisimama ghafla na shughuli za kawaida zikakwama katika mataifa yote duniani. Walimwengu walipata kibarua kigumu mno huku shughuli za uchukuzi wa kimataifa zikitatizika kwa njia zisizomithilika. Ikumbukwe pia kuwa masomo yalitatizika pakubwa huku viwango vyote vya shule vikifungwa.
Vituo vya afya navyo vilifurika kwa msongamano mkubwa wa watu huku wahudumu wa afya wakilemewa na idadi kubwa ya wagonjwa. Wahudumu hao walijipata kwenye wadi na vyumba wa wagonjwa mahututi na wengine wengi walifariki . Wengineo walikosa nafasi ya matibabu au ya kulazwa katika hospitali wanazohudumu.
Uchumi uliathirika pakubwa. Watu wengi walipoteza kazi zao. Wengine walitumwa nyumbani kwa likizo bila malipo nao wengine wakikatwa mishahara kwa asilimia kubwa. Biashara nazo hazikusazwa na gonjwa hili kwani nyingi zilifungwa wengine wakipata hasara chungu nzima. Benki zilijipata kwa njia panda kwa wateja kushindwa kulipa mikopo.
Usisahau kuwa maelfu ya watu walipoteza maisha yao huku wengine wengi wakiendelea kukabiliana na makali ya ugonjwa wa Covid-19 ambayo kwa sasa ni uhakika kuwa umejua kuwa ndio ninaozungumzia. Kenya, kama mataifa mengine ulimwenguni inaendelea kukabiliana na janga hili.
Miongoni mwa dalili za mapema za maambukizi ya gonjwa hili ni kukohoa, kushindwa kupumua au ugumu wa kupumua, joto jingi au baridi kali mwilini ,maumivu ya misuli au mwili, kutapika au kuendesha, kupoteza hisia za kuonja na kunusa miongoni mwa mengine. Yeyote anayeonyesha dalili hizi anashauriwa kujitenga na kwenda hospitalini mara moja.
Ni muhimu kujilinda dhidi ya virusi hivi. Vaa barakoa kila wakati unapoenda kwenye watu. Kumbuka kuosha mikono yako kwa maji yanayotiririka na sabuni au kuitakasa. Epuka mikusanyiko ya watu na uzingatie umbali wa mita moja unapokumbana na watu. Kaa nyumbani kama inawezekana. Wenye magonjwa mengine kama shinikizo ya damu, ukimwi, saratani,kisukari miongoni na pia watu umri wa juu wanashauriwa na wataalamu wa afya wawe makini zaidi kwani wamo hatarini zaidi.
Hebu tugeukie mikakati mbali mbali iliyowekwa na serikali ya Kenya tangu kuliporipotiwa kisa cha kwanza nchini. Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule. Kando na kufungwa huko, kafyu ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi iliwekwa hapo awali, hatua iliyolegezwa baadaye.
Kufungwa kwa uchukuzi wa kimataifa ulitangazwa huku uchukuzi nchini ukidhibitiwa kwa kupunguzwa kwa idadi ya watu kwenye uchukuzi wa uma. Mikusanyiko ya watu ulipigwa marufuku nazo kanisa zikifungwa japo kwa muda. Idadi ya watu katika arusi na mazishi ulipunguzwa mno.
Maeneo ya burudani pia yalifungwa kwa muda nayo maeneo ya maabadini yalifungwa miongoni
mwa mikakati mingine.
Baada ya miezi kadhaa, makali ya janga hili tandavu yalizidi kuwakumba wakenya huku kufungwa wa nchi kukiendelea kuathiri shughuli ya kawaida za kujikimu. Serikali iliweka mikakati ya kuinua uchumi. Wakenya wa viwango vya chini walitumiwa pesa za kujikimu huku wafanyibiashara wadogo wakiinuliwa kwa mikopo. Serikali pia ilizirai benki kuzungumza na wadeni
wao na kuwasogezea nya kati za kulipa. Ikumbukwe pia serikali ilipunguza au ushuru kwa Wa kenya wenye kipato cha chini. Serikali pia ililazimika kulegeza mika kati kadhaa ili kuwapa Wakenya nafasi ya kujichumia. Saa za Kafyu zilipunguzwa huku uchukuzi wa kitaifa na kimataifa ukifunguliwa upya. Shule pia zilianza kufung uliwa japo kwa wata hiniwa. Wamiliki wa maeneo ya burudani walinufaika na kufunguliwa kwa maeneo hayo. Viongozi wa kidini na wafuasi wao walikuwa na kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuwafungulia maeneo ya kuabudu.
Wa kenya wanaendelea kuhimizwa kufuata kanuni za wizara ya Afya dhidi ya Covid -19. Hii inaendelea huku Wakenya wa kilaumiwa kwa kutovaa barakoa, kuendelea kutangamana katika mikutano ya kisiasa, kutoosha wala kutakasa mikono,kutozingatia saa za kafyu miongoni mwa mengine.
Ulimwengu unaendeleza mchakato wa kutafiti na kutafuta chanjo ya korona huku baadhi ya mataifa wa kitangaza kupiga hatua kubwa na kwamba tutakwamuliwa hivi karibuni. Kujilinda kunabaki kuwa chanjo kuu.
Maswali
a. Thibitisha kwamba Covid-19 umezia utangamano wa kimataifa. (Alama 1)
b. Eleza kinaya inayojitokeza kwa Covid-19 na wa hudumu wa afya. (Alama 1)
c. Covid -19 umesababisha madhara mengi ya kiuchum i. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja tatu. (Alama 3)
d. Taja dalili zozote mbili za maambukizi ya virusi vya korona. (Alama 1)
e. Eleza matendo matatu kulingana na kifungu hiki ambayo yanamweka mtu kwenye hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu (Alama 3)
f. Taja mikakati miwili iliyowekwa na serikali ya Kenya kukabiliana na virusi hivi. (Alama 2)
g. Serikali ya Kenya ililegeza mikakati yake vipi? (Alama 1)
h. Eleza maana ya maneno yafutayo jinsi yalivyotumika kifunguni (Alama 2)
i. Kafyu
ii. Mchakato
- UFUPISHO – Alama 15.
Katika ulimwengu wa utandawazi, mitandao ya kijamii imekuwa na umuhimu sana. Dunia imekua kwa miaka mingi na kuendelea huko kumechangiwa pakubwa na mitandano ya kijamii.
Miongoni mwa mitambao ya kijamii ni kama vile Facebook, Twitter, YouTube, Skype, Instagram, Whatsapp, zoom miongoni mwa mengine.
Mitandao ya kijamii imerahisisha mawasiliano. Imekuwa rahisi kwa kuwasiliana bila kukutana uso kwa uso. Fauka ya hayo, biashara kitaifa na kimataifa imemarishwa na mitandao ya kijamii. Wafanyabiashara wanaweza kufanya mauzo ya bidhaa zao kupitia mitandao hii na kukutana na wateja mitandaoni. Ni muhimu pia kutambua kuwa, mitandandao ya kijamii hukuza umoja na ushirikiano wa watu na vile uzalendo. Watu wanatangamana mitandaoni na hata kuwa marafiki. Huko kunaondoa hisia za kikabila ambazo ndizo zimebababisha uhasama mkubwa.
Mitandao ya kijamii imezidi kukuza na kuendeleza demokrasia. Katika michakato ya kisiasa, wapiga kura wanaweza kujadili na kudadisi sera za wawaniaji wa viti mbali mbali na kufanya maamuzi mazuri. Wanasia pia wanaweza kuuza sera zao mitandaoni. Isitoshe, elimu imeimarishwa pakubwa na mitandao ya kijamii.
Walimu wanaweza kuwafundisha wanafunzi moja kwa moja kwa mitandao ya Kijamii. Zoom kwa mfano hutumika kuwa na mikutano na hata kufundisha. Wanafunzi pia hupata ufafanuzi wa mada mbali mbali kwa kutembelea tofuti na mitandao mbali mbali.
Ikumbukwe mitandao ya Kijamii ni nyenzo muhimu ya kueneza habari. Kando na utangazaji magazetini, runingani au redioni, habari nyingi tu hupitishwa katika mitandao kama vile facebook, Twitter, YouTube na kadhalika. Habari za kimataifa pia hueneza zaidi mitandaoni.
Wasanii wengi wamenufaika kwa mitandao hii kama nyenzo ya kipato cha kila siku,hivyo basi imeunda nafasi za ajira. Mitandao ya kijamii pia imetoa nafasi pana ya burudani kwani watu wengi hupata kufurahishwa na kuchekeshwa na wasanii mitandaoni humo.
Ingawa mitandao ya Kijamii ina faida chungu nzima, kuna hasara zake vile vile. Vijana, hata wenye umri wa miaka chini ya kumi na nane wamejiingiza kwa mapenzi. Hii imetokana na shinikizo mitandaoni ikiwemo mitandao ya video za ngono. Kanda na hayo, mitandao hii imesababisha utovu wa maadili. Vijana kwa wazee wanaiingia kwenye mitandao hii na hata kutazama filamu, nyimbo na video mbali mbali zisizofaa. Watu wanaweza kuvalia vibaya ama hata kuzungumza lugha chafu. Matukio ni kuiga tabia hizo.
Utapeli ni mwingi mitandaoni. Waja huhadaiwa na kutapeli maelfu kwa mamilioni ya pesa humo. Hii inasabababisha hasara kubwa. Watu wanaweza pia kueneza habari za uwongo mitandaoni na kusababisha mizozo. Watu binafsi wanaweza kupatwa na usumbufu wa kiakili na wengine hata kujitoa uhai. Ni muhimu pia kutambua uzembe na uvivu kama hasara inayosababishwa na mitandao ya Kijamii. Vijana wengi huwa tu kwa simu na vipakatalishi siku kutwa na hata usiku kucha bila kufanya kazi ama hata kusoma. Uchochezi wa kisiasa huenezwa humo pia. Watu ambao wangeishi kwa amani huanza vita kutokana na uchochezi mitandaoni. Hii inatinga amani ya Kijamii.
Mitandao ya Kijamii hukumbwa na changamoto nyingi. Moja ni ukosefu wa nguvu za umeme. Si watu wote wanaweza kupata nguvu hizi ili simu na vipakatilishi vipate kutumika. Upungufu wa fedha kutokana na ufukara husababishwa watu kukosa kununua simu au vipakatilisha au hata kukosa pesa za mjazo. Zaidi ya hayo ni kutoenea vya kutosha kwa mitandao mbali mbali na hivyo kutowafikia watu wote. Sera za kudhibiti matumizi matumizi ya mitandao ya Kijamii zingali ni finyu na changamamoto za kisheria. Ni muhimu kutumia mitandao hii kwa manufaa yetu wala si kutudhuru.
Maswali
a. Fafanua faida za mitandao ya Kijamii kwa maneno 100 ( Alama 9,utiririko 1) Matayarisho
Nakala safi
b. Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 90-100 (Alama 6,utiririko 1) Matayarisho
Nakala safi
- SARUFI
I. Tofautisha kati ya ala tuli na ala sogezi kwa kutolea mifano moja moja (AI. 2) Il. Tambua sauti zenye sifa zifuatazo : (AI. 2)
i. irabu ya chini wastani
ii. Sauti ambayo ni irabu na konsonanti vile vile
iii. Kizuiwa-Kikwamizwa
iv. Sauti tandaze ya mbele ,kati ya ulimi
b. Eleza tofauti iliyopo kati ya silabi wazi na silabi funge ( AI.1)
C. Tunga sentensi yenye kiunganishi cha masharti (AI. 1)
d. Geuza kirejeshi katika sentensi ifuatayo ili kuleta dhana ya hali ya mazoea (AI.1)
Wanafunzi ambao wanasoma kwa bidii watatuzwa
e. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo : (AI. 1)
Pika chakula kingine
f. Kwa kuzingatia uamilifu, taja kwa kutolea mifano aina zozote nne za sentensi za Kiswahili
(AI. 2)
g. Tilia shada katika maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo : (AI. 1)
i. Alifanya kazi yake barabara
ii. Mwimbaji alijinunulia ala za muziki.
h. Yakinisha kwa wastani (AI. 2)
Janajike lile halijanunua majitabu mazuri
i. Tunga sentensi ya neno moja yenye viambajengo vifuatavyo : (AI. 2)
Nafsi ya pili wingi,mzizi, kauli ya kutendesha, kauli ya kutenda , ‘o’rejeshi tamati
j. Fafanua miundo mitatu ya ngeli ya A-WA kwa kutolea mifano mahususi (AI. 3)
k. Ainisha viambishi awali na tamati ; (AI. 2) Waliwao
Msioabudu
I. Tambua aina za shamirisho; (AI. 3)
Mama mzee alijengewa nyumba ya kifahari na mjukuwe kwa mawe
m. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo (AI. 3)
Mwalimu huyo alikuwa akiandika kitabu kikubwa mno jana jioni.
n. Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno “kaa” (AI. 2)
o. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (AI. 4)
Wakulima wakipata pesa wataanza kazi
p. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi “-ji” (AI. 2)
q. Eleza matumizi ya kibainishi kwa kutolea mifano katika sentensi (AI. 2)
r. Andika kwa usemi halisi (AI. 3)
Mwalimu alishangaa na kutaka kujua kwa nini wanafunzi hawakuwa wameelewa mada hiyo
siku hiyo.
- ISIMUjAMII
a. Eleza maana za istilahi zifuatazo : (Alama 2)
i. sajili
ii. lahaja
b. Taja nadharia tatu za chimbuko la Kiswahili (Alama 3) C.
i. Eleza maana ya dhana usanifishaji (Alama 1)
ii. Fafanua sababu mbili za usanifishaji wa Kiswahili. (Alama 2)
d. Eleza dhima mbili za lugha lugha rasmi. (Alama 2)
Mwongozo wa Kusahihisha
- Ufahamu
a. Thibitisha kwamba Covid-19 umezia utangamano wa kimataifa. (Alama 1)
• Shughuli za kimataifa zilitatizika kwa njia zisizomithilika
b. Eleza kinaya inayojitokeza kwa Covid-19 na wa hudumu wa afya. (Alama 1)
• Wahudumu wa afya walikosa nafasi ya matibabu au nafasi ya kulazwa katika hospitali wanazohudumu wenyewe.
c. Covid -19 umesababisha madhara mengi ya kiuchumi. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja tatu. (Alama 3)
• Watu wengi kupoteza kazi zao.
• Watu wengine kutuma kwa likizo bila malipo.
• Wengine kukatwa mishahara kwa asilim ia kubwa.
• Biashara nyingi kufungwa nyingi zikipata hasara chungu nzima.
• Benki kuathirika kwa wateja kushindwa kulipa mikopo.
d. Taja dalili zozote mbili za maambukizi ya virusi vya korona. (Alama 1)
• Kukohoa
• Kushindwa kupumua au ugumu wa kupumua
• Joto jingi au baridi kali mwilini
• Maumivu ya misuli au mwili,
• Kutapika au kuendesha, kupoteza hisia za kuonja na kunusa
e. Eleza matendo matatu kulingana na kifungu hiki ambayo yanamweka mtu kwenye hatari
ya maambukizi ya ugonjwa huu (Alama 3)
• Kutovaa barakoa kila wakati unapoenda kwenye watu.
• Kutokuosha mikono yako kwa maji yanayotiririka na sabuni au kuitakasa.
• Kwenda kwenye mikusanyiko ya watu.
• Kutozingatie umbali wa mita moja unapokumbana na watu.
f. Taja mikakati miwili iliyowekwa na serikali ya Kenya kukabiliana na virusi hivi. (Alama 2)
• Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule.
• Kafyu ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi iliwekwa hapo awali
• Kufungwa kwa uchukuzi wa kimataifa ulitangazwa
• Kudhibitiwa kwa uchukuzi nchini kwa kupunguzwa kwa idadi ya watu kwenye uchukuzi wauma.
• Mikusanyiko ya watu ulipigwa marufuku
• Kanisa kufungwa japo kwa muda.
• Idadi ya watu katika arusi na mazishi kupunguzwa mno.
• Maeneo ya burudani pia yalifungwa kwa muda
g. Serikali ya Kenya ililegeza mikakati yake vipi? (Alama 1)
• Saa za Kafyu zilipunguzwa
• Uchukuzi wa kitaifa na kimataifa ulifunguliwa upya.
• Shule pia zilianza kufunguliwa japo kwa watahiniwa.
• Kufunguliwa kwa maeneo ya burudani
• Maeneo ya kuabudu yalifunguliwa japo kwa masharti ya kiafya.
h. Eleza maana ya maneno yafutayo jinsi yalivyotumika kifunguni (Alama 2)
i. Kafyu
- Ufupisho
• Amri ya kutotoka nje nyakati fulani haswa usiku hadi asubuhi kama ile ya
usiku hadi asubuhi
ii. Mchakato
• Hatua za kufuata wakati kufanya jambo kama hatua za kutafuta za kutafuta chanjo
a. Faida za mitandao ya kijamii
• Mitandao ya kijamii imerahisisha mawasiliano.
• Biashara kitaifa na kimataifa imemarishwa na mitandao ya kijamii.
• Ni muhimu pia kutambua kuwa, mitandandao ya kijamii hukuza umoja na
ushirikiano rva watu na vile uzalendo.
• Mitandao ya kijamii imezidi kukuza na kuendeleza demokrasia.
• Walimu wanaweza kuwafundisha wanafunzi moja kwa moja kwa mitandao ya Kijamii (Huimarisha elimu.
• Ikumbukwe mitandao ya Kijamii ni nyenzo muhimu ya kueneza habari.
• Habari za kimataifa pia hueneza zaidi mitandaoni.
• Wasanii wengi wamenufaika kwa mitandao hii kama nyenzo ya kipato cha kila siku,hivyo basi imeunda nafasi za ajira.
• Mitandao ya kijamii pia imetoa nafasi pana ya burudani kwani watu wengi hupata
kufurahishwa na kuchekeshwa na wasanii mitandaoni humo.
Hoja zozote 8 (1*8)
b. Fupisha aya tatu za mwisho
• Mitandao ya Kijamii ina hasara kando na kuwa na faida nyingi
• Vijana, hata wenye umri wa miaka chini ya kumi na nane wamejiingiza kwa mapenzi.
• Kando na hayo, mitandao hii imesababisha utovu wa maadili.
• Utapeli ni mwingi mitandaoni.
• Watu wanaweza pia kueneza habari za uwongo mitandaoni na kusababisha mizozo.
• Ni muhimu pia kutambua uzembe na uvivu kama hasara inayosababishwa na mitandao ya Kijamii.
• Vijana wengi huwa tu kwa simu na vipakatalishi siku kutwa na hata usiku kucha bila kufanya kazi ama hata kusoma.
• Uchochezi wa kisiasa huenezwa humo pia. Watu ambao wangeishi kwa amani huanza vita kutokana na uchochezi mitandaoni.
• Mitandao ya Kijamii hukumbwa na changamoto nyingi.
• Moja ni ukosefu wa nguvu za umeme. Si watu wote
• Upungufu wa fedha kutokana na ufukara husababishwa watu kukosa kununua simu
au vipakatilisha au hata kukosa pesa za mjazo.
• Zaidi ya hayo ni kutoenea vya kutosha kwa mitandao mbali mbali na hivyo kutowafikia watu wote.
• Sera za kudhibiti matumizi matumizi ya mitandao ya Kijamii zingali ni finyu na
changamamoto za kisheria.
• Ni muhimu kutumia mitandao hii kwa manufaa yetu wala si kutudhuru.
- Matumizi ya lugha
a.I. Tofautisha kati ya ala tuli na ala sogezi kwa kutolea mifano moja moja (AI. 2)
• Ala tuli ni ala zisizosogea wakati wa kutamka kwa mfano meno, ufizi, kakaagumu, kaakaalaini, koromeo ilhali ala sogezi ni ala za kutamkia zinazosogea wakati wa matamshi kwa mfano midomo na ulimi. (1x 2=2)
II. Tambua sauti zenye sifa zifuatazo : (AI. 2)
i. irabu ya chini wastani – /a/
ii. Sauti ambayo ni irabu na konsonanti vile vile – /w/,/y/
iii. Kizuiwa-Kikwamizwa -/ch/
iv. Sauti tandaze ya mbele ,kati ya ulimi -/e/
(1x 4= 2)
b. Eleza tofauti iliyopo kati ya silabi wazi na silabi lunge ( AI.1)
• Silabi wazi ni silabi inayoisha kwa irabu ilhali silabi funge huisha kwa konsonanti.
(lxl=l)
c. Tunga sentensi yenye kiunganishi cha masharti (AI. 1)
• Ukisoma kwa bidii utafaulu. (1x 1= 1)
d. Geuza kirejeshi katika sentensi ifuatayo ili kuleta dhana ya hali ya mazoea (AI.1) Wanafunzi ambao wanasoma kwa bidii watatuzwa
• Wanafunzi wasomao kwa bidii watatuzwa (1x 1=1)
e. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo : (AI. 1) Pika chakula kingine
• Kuongeza /ziada ya
• Badala ya /kibadaIa cha /tofauti na (i/zx 2=1)
f. Kwa kuzingatia uamilifu, taja kwa kutolea mifano aina zozote nne za sentensi za Kiswahili (AI. 2)
• Sentensi ya swali
• Sentensi ya hisia /mshangao
• Sentensi ya ombi /rai
• Sentensi ya amri
• Sentensi ya taarifa(1/2×4=2)
g. Tilia shada katika maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo : (AI. 1)
• Alifanya kazi yake ba’rabara
• Mwimbaji alijinunulia a’Ia za muziki.
(2X2=l)
h. Yakinisha kwa wastani (AI. 2)
Janajike IiIe halijanunua majitabu mazuri
• Mwanamke yule amenunua vitabu vizuri
(2 x 2=2)
Tunga sentensi ya neno moja yenye viambajengo vifuatavyo : (AI. 2)
Nafsi ya pili wingi,mzizi, kauli ya kutendesha, kauli ya kutenda , ‘o’rejeshi tamati
• Msomeshao
• Hakiki majibu ya mwanafunzi
(1x 1= 1)
j. Fafanua miundo mitatu ya ngeli ya A-WA kwa kutolea mifano mahususi (AI. 3)
• M -wa :Mtu -watu
• M -Mi :Mtume -Mitume
• Ki -Vi :Kifaru -Vifaru
• Ch -Vy :Chura -Vyura
• Kapa -Ma :Daktari -Madaktari
(1×3=3)
k. Ainisha viambishi awali na tamati ; (AI. 2)
• Waliwao – Wa – awali
-iwao -tamati (‘/2 x 2= 1)
• Msioabudu – msio -awali
u -kiambishi tamati (‘/2 x 2=1)
l. Tambua aina za shamirisho; (AI. 3)
Mama mzee alijengewa nyumba ya kifahari na mjukuwe kwa mawe
• Mama mzee -kitondo nyumba ya kifahari -kipozi mawe -ala
(1x 3=3)
m. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo (AI. 3)
Mwalimu huyo alikuwa akiandika kitabu kikubwa mno jana jioni.
• RN-MwaIimu huyo
• RT-alikuwa akiandika
• RN -kitabu kikubwa
• RV- Kikubwa mno
• RE -mno jana jioni
• RT -alikuwa akiandika kitabu kikubwa mno jana jioni
• RN – kitabu kikubwa mno j Atambua aina zozote 6 (‘/2 x 6=3)
n. Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno “kaa” (AI. 2)
• Mnyama wa majini
• Kitendo cha kuketi
• Pande la kuni lililochomwa
• Kushinda mahali fulani
(1×2=2)
o. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (AI. 4) Wakulima wakipata pesa wataanza kazi
p. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi “-ji” (AI. 2)
• Uundaji wa nomino kutoka kitenzi – uimbaji, mwimbaji
• Mtendwa – amejipikia
• Ukubwa – jitoto, jitu Atungie sentensi MOJA (lx2=2)
q. Eleza matumizi ya kibainishi kwa kutolea mifano katika sentensi (AI. 2) Ritifaa
• Ufupishaji wa maneno/tarakimu – ‘ndo badala ya ndio , ’63-1963
• Kuonyesha sauti ya ving’ong’o – ng’ombe
• Kuonyesha silabi iliyotiliwa mkazo – ba’rabara
(1×2=2)
r. Andika kwa usemi halisi (AI. 3)
Mwalimu alishangaa na kutaka kujua kwa nini wanafunzi hawakuwa wameelewa mada hiyo
siku hiyo (AI. 3)
• “Ala! Kwa nini hamjaelewa mada hii leo? ” Mwalimu akauliza.
Hakiki matumizi ya vihisishi vinginevyo (1x 3=3)
- ISIMUjAMII
a. Eleza maana za istila hi zifuatazo : (Alama 2)
i. sajili – ni muktadha mbali mbali ya matumizi ya lugha
ii. la haja – ni vilugha vidogo vidogo vinavyotokana na lugha moja kuu.
(1xl=2)
b. Taja nadharia tatu za chimbuko la Kiswahili (Alama 3)
i. Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya Kibantu
ii. Kiswahili ni la haja ya Kiarabu
iii. Kiswahili ni lugha ya mseto
c.i. Eleza maana ya dhana usanifishaji (Alama 1)
• Ni uteuzi na uimarishaji wa lahaja moja ya lugha miongoni mwa lahaja
nyingine ili kutumika katika shughuli rasmi. (1×1=1)
ii. Fafanua sababu mbili za usanifishaji wa Kiswahili . (Alama 2)
• Kuwepo kwa lahaja nyingi za Kiswahili
• Kulikuwa na hati tofauti zilizotumiwa kuandika Kiswahili
• Shughuli mbali mbali za kidini
• Haja ya kusawazisha maandishi ya kitaaluma
• Haja ya kuwa na lugha moja ya mawasiliano na elimu (1×1=2)